Maonyesho ya kimataifa ya zana za mashine yaanza Shanghai, China (6)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Machi 05, 2025
Maonyesho ya kimataifa ya zana za mashine yaanza Shanghai, China
Watembeleaji wakitazama mashine yenye uwezo wa kugeuka inayooneshwa kwenye Maonyesho ya Kimataifa ya Zana za Mashine ya Shanghai, mashariki mwa China, Machi 3, 2025. (Xinhua/Fang Zhe)

SHANGHAI - Maonyesho ya Kimataifa ya Zana za Mashine ya Shanghai Mwaka 2025 yameanza Jumatatu kwenye Kituo cha Kitaifa cha Maonyesho na Mikutano mjini Shanghai, mashariki mwa China.

Maonesho hayo yameshirikisha kampuni takriban 1,200 za ndani na nje ya China kutoka sekta husika, na kuweka mkazo katika kuonesha mipango ya uchakataji maalum kwa sekta zenye mahitaji makubwa kama vile magari yanayotumia nishati mpya, utengenezaji wa vifaa vya kielektroniki, na zana na vifaa vya usafiri wa anga.

Watembeleaji wa maonyesho hayo wanapata fursa ya kutazama maonyesho yanayoonesha sehemu za kiini za mashine ya udhibiti wa kidigitali , vifaa vya uchakataji wa leza, zana za kuponda kutengeneza vitu bapa, pamoja na aina mbalimbali za bidhaa husika na teknolojia za kisasa za hali ya juu.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha