Kongamano la Mawasiliano ya Simu za Mkononi Duniani Mwaka 2025 laanza likijikita katika AI na 5G (6)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Machi 05, 2025
Kongamano la Mawasiliano ya Simu za Mkononi Duniani Mwaka 2025 laanza likijikita katika AI na 5G
Mtu akitazama simu janja ya kukunjika mara tatu ya Kampuni ya HUAWEI kwenye Kongamano la Mawasiliano ya Simu za Mkononi Duniani Mwaka 2025 mjini Barcelona, Hispania, Machi 3, 2025. (Xinhua/Zhao Dingzhe)

BARCELONA - Kongamano la Mawasiliano ya Simu za Mkononi Duniani (Mobile World Congress, MWC) Mwaka 2025 lenye kaulimbiu ya "Jumuisha, Unganisha, Unda," ambalo limepangwa kufanyika kwa siku nne, limefunguliwa mjini Barcelona, Hispania Jumatatu, likileta pamoja viongozi wa tasnia, watunga sera, na wavumbuzi wa teknolojia ili kuchunguza maendeleo katika 5G, Akili Mnemba (AI), na uunganishaji intaneti wa hali ya juu.

Kongamano hilo ambalo limeandaliwa na GSMA kwenye kituo cha maonyesho cha Fira Gran Via, linasisitiza muunganisho wa teknolojia za mawasiliano ya simu za mkononi na zile zinazoendeshwa na AI.

Mats Granryd, mkurugenzi mkuu wa GSMA, amezungumzia matumizi ya haraka ya 5G duniani, akibainisha kuwa miunganisho imefikia bilioni 2, ikiifanya kuwa kizazi cha mawasiliano ya simu za mkononi kinachokua kwa kasi zaidi hadi sasa.

"Sasa ni wakati wa kuondoa vizuizi na kubonyeza kitufe cha kuharakisha ukuaji," amesema.

GSMA pia imetoa Ripoti yake ya Uchumi wa Mawasiliano ya Simu za Mkononi Mwaka 2025, ambayo imeonesha kuwa teknolojia na huduma za mawasiliano ya simu za mkononi zilichangia asilimia 5.8 ya Pato la Dunia mwaka 2024, sawa na dola za Kimarekani trilioni 6.5. Kiasi hicho kinakadiriwa kuja kufikia dola za Kimarekani trilioni 11, au asilimia 8.4 ya Pato la Dunia, ifikapo mwaka 2030, ikichochewa na upanuzi wa 5G, Intaneti ya Vitu (IoT), na AI.

MWC 2025 imevutia waonyeshaji bidhaa zaidi ya 2,800 na wazungumzaji 1,200, huku waandaaji wakitarajia wahudhuriaji zaidi ya 100,000. Kampuni zaidi ya 300 za China, zikiwemo China Mobile, China Unicom, China Telecom, Huawei, ZTE, Lenovo, na Xiaomi, zinaonyesha ubunifu wao wa hivi punde.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha