Mashamba ya chai kote wilayani Wuyi yaingia majira ya mavuno

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Machi 06, 2025
Mashamba ya chai kote wilayani Wuyi yaingia majira ya mavuno
Wakulima wakichuma majani ya chai kwenye mashamba ya chai ya Wangzhai ya Wilaya ya Wuyi ya Mji wa Jinhua, Mkoa wa Zhejiang, Mashariki mwa China, Machi 5, 2025.

Majira ya mchipuko yanapowadia, mashamba ya chai kote wilayani Wuyi, Mkoa wa Zhejiang, Mashariki mwa China yameingia katika majira ya mavuno.

Katika miaka ya hivi katibuni, wilaya hiyo ya Wuyi imekuwa ikiendeleza shughuli ya chai ambayo imekuwa nguzo ya shughuli zake zote. Hadi kufikia mwishoni mwa mwaka 2024, ukubwa wa jumla wa eneo la mashamba ya chai katika wilaya hiyo umefikia mu 125,700 (hekta takriban 8,380). Wakulima zaidi ya 60,000 wameweza kufaidika moja kwa moja na biashara husika za chai. 

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha