Habari picha ya msanifu wa kike anayeongoza mradi wa ndege ya C929 ya China

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Machi 07, 2025
Habari picha ya msanifu wa kike anayeongoza mradi wa ndege ya C929 ya China
Zhao Chunling akionekana katika picha kwenye taasisi ya utafiti ya Shirika la Ndege za Kibiashara la China (COMAC) mjini Shanghai, Mashariki mwa China, Machi 5, 2025. (Xinhua/Liu Ying)

Zhao Chunling, msanifu mkuu wa ndege C929 yenye umbo pana iliyoundwa kikamilifu na China yenyewe, ni msanifu mkuu wa kwanza wa kike katika sekta ya anga ya China anayeongoza mradi mkubwa wa ndege wa kitaifa wa China.

Zhao alianza kazi yake katika tasnia ya anga mara tu baada ya kuhitimu. Mwaka 2009, alijiunga na COMAC na kubeba jukumu muhimu katika usanifu, uundaji na majaribio ya ndege za C909 na C919. Mwaka 2023, aliteuliwa kuwa msanifu mkuu wa ndege za C929, akiongoza timu yake kusukuma vikomo vya uundaji wa ndege za kibiashara wa China.

"Nafasi, majukumu, na changamoto zilibadilika baada ya muda, lakini shauku yangu kwa usafiri wa anga na dhamira yangu isiyo na woga havijawahi kuyumba," Zhao amesema.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha