

Lugha Nyingine
Ripoti ya kazi ya serikali ya China yatolewa katika Breli kusaidia wajumbe wenye ulemavu wa macho (5)
![]() |
Mjumbe Wang Yongcheng (katikati) akigusa toleo la Breli la ripoti ya kazi ya serikali kwenye ufunguzi wa Mkutano wa pili wa Bunge la 14 la Umma la China, Machi 5, 2024. (Xinhua) |
Katika mikutano mikuu miwili ya China inayoendelea mjini Beijing, yaani mkutano wa mwaka wa Bunge la 14 la Umma la China na ule wa Kamati ya 14 ya Kitaifa ya Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la China, toleo la Breli (maandishi ya watu wenye ulemavu wa macho) la ripoti ya kazi ya serikali ya nchi hiyo imetolewa kwa mara ya kwanza kwa wajumbe wa Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la China.
Wakati wa mchana wa jana Alhamisi, tarehe 5, Machi, mjumbe wa baraza hilo, Li Qingzhong kwenye kikao cha kikundi cha wajumbe wa sekta ya ustawi wa jamii na huduma za jamii, mahsusi aliomba kila mjumbe kuzingatia ripoti hiyo maalumu ya kazi ya serikali aliyokuwa ameishika mkononi wakati akizungumza.
Kutoka kutolewa kwa mara ya kwanza kwa toleo la Breli la ripoti ya kazi ya serikali kwenye mkutano wa mwaka wa Bunge la Umma la China mwaka jana, hadi utolewaji huo wa mara ya kwanza wa toleo la Breli la ripoti hiyo kwa wajumbe wa Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la China mwaka huu, badiliko limeeleza vizuri demokrasia yenye umaalum wa China.
Toleo la Breli la nyaraka za mikutano mikuu hiyo miwili linatoa huduma bora kwa wajumbe na watu wenye ulemavu wa macho, ikiwawezesha kuwa na dhamira zaidi katika kutekeleza majukumu yao.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma