

Lugha Nyingine
Viongozi wa China wajiunga na watungaji wa sheria na washauri wa kisiasa wa kitaifa katika mashauriano na mijadala
BEIJING - Viongozi waandamizi wa China Li Qiang, Zhao Leji, Wang Huning, Cai Qi, Ding Xuexiang na Li Xi Alhamisi walihudhuria vikao vya majadiliano katika mkutano wa tatu wa Bunge la 14 la Umma la China na vikundi vya majadiliano kwenye mkutano wa tatu wa Kamati ya 14 ya Kitaifa ya Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la China (CPPCC).
Waziri mkuu Li Qiang alishiriki kwenye majadiliano ya kikundi cha wajumbe wa Mkoa wa Hebei wanaohudhuria Mkutano wa tatu wa Bunge la 14 la umma, ambapo amehimiza mkoa huo kutumia fursa ya kufanya ushirikiano na uratibu katika maendeleo ya Beijing-Tianjin-Hebei ili kujipatia maendeleo zaidi.
Amesema kuwa ni muhimu kusukuma mbele ujenzi wa Eneo Jipya la Xiong'an kwa vigezo vya juu na viwango vya juu, kuboresha miundombinu na huduma za umma, na kujenga mazingira yenye hali nzuri ya kufaa kwa kuishi na kufanya kazi.
Siku hiyo asubuhi, Waziri Mkuu huyo pia alishiriki katika kikao cha pamoja cha kikundi cha washauri wa kisiasa kutoka sekta za uchumi na kilimo. Amesisitiza kuwa, ili kutimiza malengo na majukumu yaliyopangwa kwa mwaka huu, kufanya udhibiti wa mambo ya jumla ni lazima kuwa na upeo mpana wa kutupia macho siku za baadaye, kulenga kazi husika kwa usahihi ili kupata ufanisi zaidi.
Li Qiang pia amesema lazima kufanya juhudi za kuhimiza ukuaji wa miji na ustawishaji wa vijiji.
Mwenyekiti wa Bunge la umma la China Zhao Leji alishiriki katika kikao cha pamoja cha washauri wa kisiasa kutoka Chama cha Zhi Gong cha China, Shirikisho Kuu la China la Wachina Waliorejea kutoka Ng'ambo na wajumbe wa mashirika ya urafiki na nchi za nje, ambapo amewahimiza kuimarisha juhudi katika kazi za kutoa mashauriano, kuthibitisha ripoti na nyaraka na kufanya usimamizi wa kidemokrasia.
Mwenyekiti wa Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la China Wang Huning alipofanya mazungumzo na washauri wa kisiasa kutoka makundi ya dini mbalimbali, aliwahimiza kuendeleza dini kwa utaratibu katika muktadha wa China, na kuanzisha hatua kwa hatua mafundisho ya dini yanayoendana na hali halisi ya nchi ya China.
Cai Qi, mjumbe wa Sekretarieti ya Kamati Kuu ya Chama, alishiriki katika kikao cha pamoja cha washauri wa kisiasa kutoka sekta za sayansi ya jamii pamoja na vyombo vya habari. Amewahimiza kutumia nguvu bora za sekta zao na kutoa maoni na mapendekezo yao kwa ajili ya kuendeleza ujenzi wa mambo wa kisasa wa China.
Naibu Waziri Mkuu wa China Ding Xuexiang alihudhuria kikao cha pamoja cha washauri wa kisiasa kutoka mikoa ya utawala maalum ya Hong Kong na Macao, amesisitiza umuhimu wa kushikilia "nchi moja, mifumo miwili" na kulinda kithabiti ustawi na utulivu wa mikoa hiyo miwili.
Li Xi, katibu wa Kamati Kuu ya Ukaguzi wa Nidhamu ya CPC, alihudhuria kikao cha pamoja cha washauri wa kisiasa kutoka Umoja wa Vijana wa Kikomunisti wa China na Shirikisho Kuu la Vijana la China, Shirikisho Kuu la Wafanyakazi la China, na Shirikisho Kuu la Wanawake la China.
Amewahimiza washauri hao wa kisiasa wawe na hamasa zaidi katika kutoa maoni na mapendekezo juu ya kuimarisha zaidi mageuzi kwa kina, kuhimiza maendeleo ya sifa bora , na kuandaa Mpango wa 15 wa Maendeleo ya Uchumi na Jamii ya Miaka Mitano (2026-2030), na masuala mengine. Pia amesisitiza kushikilia msimamo wa kutoa shinikizo la juu kwa vitendo vyote vya kukiuka nidhamu na kufanya ufisadi.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma