

Lugha Nyingine
Mabanda ya kilimo cha teknolojia za kisasa yasaidia mavuno ya mboga za majani wilayani Xiaochang, China
Kwa sasa ni msimu wa kilimo cha majira ya mchipuko nchini China. Mboga za majani aina zaidi ya 100 zimepandwa kwenye banda la kilimo cha kisasa lenye joto mwafaka la Eneo Maalum la Kilimo cha Kisasa la Jiufeng katika Wilaya ya Xiaochang, Mji wa Xiaogan, Mkoa wa Hubei, China, na wafanyakazi wana pilika nyingi kusimamia ukuaji wa mboga hizo za majani.
Kwa kupitia jukwaa mahiri la data za kilimo kwenye mlango wa banda hilo, data za kimazingira kama vile halijoto na unyevunyevu zinaweza kuonekana dhahiri. Wataalam wa kilimo hutumia data hizo kuunganisha mizunguko tofauti ya ukuaji wa mboga za majani kuandaa mchanganyo wa virutubisho.
Kilimo hicho cha kiteknolojia si tu kinafanya kiwango cha mboga za majani kuwa bora, bali pia kinaongeza mavuno mara mbili. Kwa mfano, wastani wa mavuno ya nyanya ndogo zinazopandwa kwa njia ya kawaida kwa kila mu ni kilo 4,000, lakini hapa mavuno yanaweza kufikia kilo 12,000 kwa kila mu.
Katika miaka ya hivi karibuni, Wilaya hiyo ya Xiaochang imeanzisha maeneo maalum ya kilimo cha kisasa cha mboga za majani ili kuboresha sekta ya upandaji mboga za majani. Ikihamasishwa na sekta hiyo ya kilimo cha kisasa cha mboga za majani, watu zaidi ya 20,000 walioko vijiji tisa vya utawala karibu na Eneo hilo Maalum la Kilimo cha Kisasa la Jiufeng wamepata ajira na kuongeza mapato yao.
Watu mjini Lhasa, China wafanya maandalizi ya sikukuu ijayo ya Mwaka Mpya wa Watibet
Mandhari na wanyama katika Hifadhi ya Taifa ya Nairobi, Kenya
Habari Picha: Kituo cha Matengenezo yote ya Ndege katika sehemu moja mjini Haikou, China
Dunhuang katika Mkoa wa Gansu wa China yakaribisha maendeleo mapya
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma