Viongozi wa China wahudhuria vikao vya majadiliano katika mkutano wa mwaka wa Bunge la China (2)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Machi 08, 2025
Viongozi wa China wahudhuria vikao vya majadiliano katika mkutano wa mwaka wa Bunge la China
Cai Qi, mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na mjumbe wa sekretariati ya Kamati Kuu ya CPC akishiriki kwenye kikao cha majadiliano cha kundi la wajumbe wa Bunge la 14 la Umma la China kutoka Mkoa Qinghai katika mkutano wa tatu wa Bunge hilo la 14 mjini Beijing, Mji Mkuu wa China, Machi 7, 2025.. (Xinhua/Shen Hong)

BEIJING - Viongozi waandamizi wa China Ijumaa walihudhuria vikao vya majadiliano katika mkutano wa tatu wa Bunge la Umma la 14 la China, unaoendelea mjini Beijing, mji mkuu wa China.

Mwenyekiti wa Kamati ya Kitaifa ya Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la China, Wang Huning ameshiriki katika kikao cha majadiliano cha kundi la wajumbe wa Bunge hilo kutoka Taiwan. Amesisitiza haja ya kutilia maanani kanuni ya kuwepo kwa China moja na Makubaliano ya mwaka 1992, na kupinga kithabiti "kujitenga kwa Taiwan" na uingiliaji wa nje.

Wang, amesisitiza maendeleo jumuishi ya kina na ya vitendo ya pande mbili za Mlango-Bahari wa Taiwan ili kuwezesha watu wa Taiwan kunufaika na fursa na mafanikio ya ujenzi wa mambo ya kisasa wa China.

Cai Qi, mjumbe wa Sekretarieti ya Kamati Kuu ya CPC, ameshiriki kwenye kikao cha majadiliano ya kundi la wajumbe wa Bunge la 14 la Umma la China kutoka Mkoa wa Qinghai. Amesisitiza haja ya kuimarisha mageuzi kwa kina, kuhimiza uboreshaji wenye ufanisi wa uchumi na ongezeko la uchumi kwa kiwango kifaacho.

Cai pia ameuhimiza mkoa huo kuimarisha uhifadhi wa ikolojia ili kulinda "mnara wa maji wa China" na kufanya ipasavyo kazi ya kiikolojia.

Naibu Waziri Mkuu Ding Xuexiang alihudhuria kwenye kikao cha majadiliano ya kundi la wajumbe wa Bunge la Umma la 14 la China kutoka Mikoa ya Utawala Maalum ya Hong Kong na Macao, mtawalia. Amebainisha kuwa China imepata maendeleo madhubuti katika ujenzi wake wa mambo ya kisasa na kupata mafanikio mapya katika kusongeza mbele "nchi moja, mifumo miwili."

Amehimiza mikoa hiyo miwili kubeba majukumu yao ya kutekeleza sera ya "nchi moja, mifumo miwili" katika zama mpya na kujitahidi kwa maendeleo makubwa zaidi.

Wang, Cai na Ding wote ni wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya CPC.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha