

Lugha Nyingine
Mfumo muhimu wa kizazi kijacho cha "jua la kutengenezwa na binadamu" la China wafaulu mchakato wa kukubaliwa
HEFEI - China imepiga hatua nyingine muhimu katika maendeleo ya kizazi kijacho cha "jua la kutengenezwa na binadamu," kwa moja kati ya mifumo yake muhimu kufaulu taratibu za ukaguzio na kukubaliwa na wataalam jana siku ya Jumapili, ikifikia maendeleo ya hali ya juu na kiwango cha uwezo wa kiuendeshaji kimataifa.
Chemba tupu ya moja-nane na mfumo wa jumla wa ufungaji umeundwa na Taasisi ya Fizikia ya Plasma ya Akademia ya Sayansi ya China (ASIPP). Ni moja ya mifumo midogo 19 ya Kituo Jumuishi cha Utafiti wa Teknolojia ya Uunganishaji (CRAFT), jukwaa ambalo wahandisi hutengeneza na kujaribu vipengele muhimu vya vinu vya nishati ya muunganisho.
Ukiwa unafanana na kipande cha chungwa, mfumo huo mpya ulioidhinishwa una sehemu ya mapishano yenye umbo la D ukiwa na gamba la safu mbili na urefu wa mita 20. Gamba hilo la chemba hiyo tupu, lililoundwa kwa chuma cha pua cha kaboni chache, lina uzito wa tani 295. Katika siku zijazo, nane kati ya hivyo "vipande vya machungwa" vitaunda muundo kamili, vikihifadhi plasma katika joto linalozidi digrii milioni 100 Celsius.
Liu Zhihong, mtafiti katika ASIPP na mwanasayansi mkuu wa mfumo huo, ameeleza kuwa chemba hiyo tupu hutumika kama kizuizi cha karibu zaidi cha usalama wa nyuklia kwenye msingi wa kinu, ikihitaji usahihi wa hali ya juu katika suala la kuchomelea, ukamilifu sahihi wa kimuundo na upenyezaji wa sumaku.
Timu ya utafiti na uundaji wa mfumo huo imetumia muongo mmoja kushinda changamoto za kiufundi katika uundaji wao wa mfumo, ikipata hataza zaidi ya 40 za uvumbuzi katika safari nzima hiyo.
"Kwa kukamilisha chemba hiyo tupu ya moja-nane, tumefahamu kikamilifu teknolojia muhimu hitajika kwa chemba tupu kamili ya toroidal kwa vinu vya muunganisho vya siku zijazo," Liu amesema, akibainisha kuwa teknolojia ya mfumo huo pia imetumika kwa viongeza kasi vya chembe, mashine za usahihi na vifaa vya kielektroniki.
Amesema, lengo kuu la jua hilo la kutengenezwa na bindamu ni kuunda muunganiko wa nyuklia kama jua, ikiwapa binadamu chanzo cha nishati safi isiyoisha na kuwezesha uchunguzi wa anga ya juu zaidi ya mfumo wa jua.
Watu mjini Lhasa, China wafanya maandalizi ya sikukuu ijayo ya Mwaka Mpya wa Watibet
Mandhari na wanyama katika Hifadhi ya Taifa ya Nairobi, Kenya
Habari Picha: Kituo cha Matengenezo yote ya Ndege katika sehemu moja mjini Haikou, China
Dunhuang katika Mkoa wa Gansu wa China yakaribisha maendeleo mapya
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma