Uhuishaji wa urithi wa kitamaduni usioshikika washika kasi katika Mji wa Fuzhou, China

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Machi 12, 2025
Uhuishaji wa urithi wa kitamaduni usioshikika washika kasi katika Mji wa Fuzhou, China
Msanii wa ufundi Chen Lizhong (wa kwanza kushoto) akiwaelekeza wanafunzi kuhusu nakshi za jiwe za Shoushan kwenye studio mjini Fuzhou, Mkoa wa Fujian, kusini mashariki mwa China, Machi 5, 2025. (Xinhua/Lin Shanchuan)

FUZHOU – Mji wa Fuzhou katika Mkoa wa Fujian, Kusini-Mashariki mwa China, ni maskani ya urithi tajiri wa kitamaduni usioshikika, ukiwemo wa nakshi za jiwe za Shoushan, sanaa zilizonakshiwa kwa behedani za Fuzhou, nakshi za mbao, na miavuli ya karatasi ya mafuta, n.k.

Katika miaka ya hivi karibuni, mji huo wa Fuzhou umekuwa ukichunguza njia mpya katika kurithisha na uvumbuzi wa urithi huo wa kitamaduni usioshikika. Kwa kujumuisha urithi huo wa kitamaduni usioshikika katika maisha ya kila siku na kuvutia vijana zaidi kujionea na kuuhisi, uhai mpya unaingizwa katika urithishaji na maendeleo yake.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha