Watu 12 wafariki na wengine 45 kujeruhiwa baada ya basi kupinduka Kaskazini Mashariki mwa Afrika Kusini (4)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Machi 12, 2025
Watu 12 wafariki na wengine 45 kujeruhiwa baada ya basi kupinduka Kaskazini Mashariki mwa Afrika Kusini
Picha hii iliyopigwa kwa simu ya mkononi ikionyesha wafanyakazi wakisafisha eneo la ajali ya basi katika Jimbo la Gauteng, Kaskazini Mashariki mwa Afrika Kusini, Machi 11, 2025. (Picha na Shiraaz Mohamed/Xinhua)

JOHANNESBURG – Watu takriban 12 wamefariki dunia na wengine 45 kujeruhiwa jana Jumanne asubuhi baada ya basi la abiria kupinduka katika Jimbo la Gauteng kaskazini mashariki mwa Afrika Kusini.

Andile Mngwevu, mjumbe wa Kamati ya Meya ya Uchukuzi katika Jiji la Ekurhuleni, amesema kuwa ajali hiyo imetokea kwenye barabara kuu ya jiji hilo karibu na Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa OR Tambo wa Johannesburg majira ya saa 12:45 asubuhi kwa saa za huko (0445 GMT).

Watu takriban 12 wamefariki kwenye eneo la tukio, na abiria 45 waliojeruhiwa wamesafirishwa hadi hospitali za karibu, alisema Mngwevu, awali wakati habari hii ikiripotiwa. "Pole zetu za dhati kwa familia za marehemu, na maombi yetu ya kuwaponya haraka wale waliofikishwa katika hospitali mbalimbali karibu na eneo hili." aliongeza.

Kwa mujibu wa Mngwevu, uchunguzi ulikuwa bado ukiendelea ili kubaini chanzo cha ajali hiyo, huku akiongeza kuwa, kama kuna magari mengine yamehusika kwenye ajali hiyo bado ilikuwa haijathibitishwa.

Msemaji wa Jiji la Ekurhuleni Zweli Dlamini ameliambia Shirika la Habari la China, Xinhua kwamba basi hilo lililohusika katika ajali hiyo lilikuwa likitoka Katlehong kuelekea Kempton Park. “Bado tupo eneo la tukio, na tunaendelea na zoezi la kutoa miili,” alibainisha alipohojiwa na Xinhua. 

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha