

Lugha Nyingine
Mwendelezaji misitu ageuza vilima kuwa vya kijani, kuongeza mapato ya wakulima kwa kutumia zaidi ya muongo
![]() |
Wu Guangrong akilisha kuku kwenye bustani ya ikolojia katika Wilaya ya Longli, Mkoa wa Guizhou, kusini-magharibi mwa China, Machi 11, 2025. (Xinhua) |
Wu Guangrong, mzaliwa wa Kitongoji cha Fangxiang katika Mkoa wa Guizhou, kusini-magharibi mwa China amekuwa akijishughulisha na tasnia ya mandhari za mazingira kwa miaka mingi tangu alipohitimu kutoka shule ya ufundi wa misitu mwaka 2001.
Akiwa na upendo maalum kwa misitu, alitia saini kwenye mkataba wa kutumia ardhi kame mlimani yenye ukubwa wa mu 4,000 (ekari kama 659) katika moja ya vijiji vya Wilaya ya Longli mwaka 2013, na hatua kwa hatua akaiendeleza na kuibadili kuwa bustani ya ikolojia hasa akipanda maua ya camellia, pamoja na miche ya kijani, matunda yenye ubora na misitu.
Hivi karibuni, bustani hiyo ya ikolojia ya Wu imekuwa nguzo ya ustawishaji wa kijiji hicho, si tu kwa kugeuza vilima visiyo na mimea kuwa vya kijani, lakini pia kutoa fursa za kazi kwa wanavijiji wenyeji.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma