Ndege iliyombeba Rais wa zamani wa Ufilipino Duterte yatua Uholanzi iliko mahakama ya ICC

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Machi 13, 2025
Ndege iliyombeba Rais wa zamani wa Ufilipino Duterte yatua Uholanzi iliko mahakama ya ICC
Ndege iliyombeba Rais wa zamani wa Ufilipino Rodrigo Duterte ikiwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Rotterdam The Hague mjini Rotterdam, Uholanzi, Machi 12, 2025. (Xinhua/Peng Ziyang)

THE HAGUE - Ndege iliyombeba Rais wa zamani wa Ufilipino Rodrigo Duterte imewasili jana Jumatano alasiri katika Uwanja wa Ndege wa Rotterdam The Hague nchini Uholanzi. Duterte, mwenye umri wa miaka 79, alikamatwa juzi Jumanne asubuhi alipokuwa akirejea Manila kutoka nje ya nchi, kufuatia hati ya kukamatwa kwake iliyotolewa na Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) kuhusu kampeni yake ya "vita dhidi ya dawa za kulevya", hatua ambayo ameitilia shaka.

Aliondoka Manila kuelekea The Hague, makao makuu ya ICC, juzi Jumanne usiku.

Katika taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa siku hiyo ya Jumatano, ICC imesema kuwa Duterte amejisalimisha chini ya ulinzi.

Makamu wa Rais wa Ufilipino Sara Duterte, ambayo ni mtoto wa rais huyo wa zamani, naye alikuwa ameondoka kuelekea Uholanzi siku hiyo ya Jumatano asubuhi. Alishawahi kusema hapo awali kwamba angeambatana na baba yake hadi The Hague kwa ajili ya mienendo ya kesi hiyo ya ICC.

Uwanja wa Ndege wa Rotterdam The Hague, ulioko kaskazini-magharibi mwa Rotterdam, uko umbali wa kilomita takriban 20 kutoka The Hague. 

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha