Kijana wa familia ya wafugaji mkoani Xinjiang, China atimiza ndoto ya kuwa rubani (2)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Machi 14, 2025
Kijana wa familia ya wafugaji mkoani Xinjiang, China atimiza ndoto ya kuwa rubani
Mirbek Tlobek (wa pili, kushoto) na mwenzake wakisafisha uwanja wa vyombo vya anga kwenye kampuni ya usafiri wa anga katika Eneo linalojiendesha la Kabila la Wakazak la Ili, Mkoa wa Xinjiang, kaskazini-magharibi mwa China, Machi 5, 2025. (Xinhua/Ding Lei)

Mirbek Tlobek, mwenye umri wa miaka 23, alizaliwa katika familia ya wafugaji wa kabila la Wakazakh katika Mkoa wa Xinjiang, kaskazini-magharibi mwa China. Tangu utotoni, alikuwa na ndoto ya kuwa rubani. Baada ya kuhitimu masomo mwaka 2023, alipata fursa ya kufanya mazoezi ya kazi katika kampuni ya usafiri wa ndege wa matumizi ya kiraia , na kisha kupata kwa mafanikio leseni za rubani wa helikopta za kibinafsi na za kibiashara.

Leo hii, Mirbek Tlobek ni rubani mtaalamu wa kuendesha helikopta katika kampuni hiyo ya usafiri wa anga huko Narat, sehemu yenye vivutio vya utalii inayokaribishwa na watu zaidi katika miaka ya hivi karibuni. Watalii humiminika huko kupanda helikopta na kufurahia mandhari nzuri ya angani.

Wakati wa kufanya usafiri angani, Mirbek Tlobek huwajulisha abiria milima na mito yenye uzuri wa aina yake mkoani Xinjiang. Pia huwaelezea simulizi za kuvutia kuhusu kujumuika pamoja kwa watu wa makabila mbalimbali, na simulizi yake binafsi ya kuwa rubani wa helikopta. Tangu alipopata leseni zake hizo za urubani, Mirbek Tlobek amefanya usafiri angani kwa helikopta kwa saa zaidi ya 430.

"Katika siku zijazo, nina matumaini ya kupata leseni ya mkufunzi ili niweze kutoa mafunzo kwa wanafunzi na kusaidia watu kama mimi kutimiza ndoto zao," amesema Mirbek Tlobek. 

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha