

Lugha Nyingine
Kituo cha Upandaji Blueberry kidijitali chaingia msimu wa mavuno Yunnan, China (4)
Ulipoanza mwezi Machi, kituo cha upandaji blueberry kidijitali katika Wilaya inayojiendeshwa ya Kabila la Wayi ya Yangbi, Mkoani Yunnan, China kiliingia msimu wa mavuno. Kwenye vibanda 11 vya kiotomatiki ndani ya kituo hicho, wanakijiji hupishana kwenye kazi za kati ya kuchuma na kufungasha matunda hayo, na kuyasafirisha hadi sehemu mbalimbali nchini humo kupitia mnyororo baridi.
Inafahamika kuwa, kituo hicho kilitumia ujenzi wa kidijitali, na kila kitu kuanzia mifumo ya maji na mbolea hadi ile ya umwagiliaji inaweza kudhibitiwa kwa mbofyo mmoja kwenye simu ya mkononi. Tofauti na njia za kijadi za upandaji, kituo hicho hutumia, njia ya upandaji mimea kwenye safu za vyombo maalum. Kila chombo huwa na dripu nne, na vyombo hivyo vimeunganishwa na mirija ya maji. Matone ya maji hudondoshwa kwenye vyombo hivyo kupitia mirija hiyo, hali ambayo si tu inadhibiti kiusahihi maji na mbolea, lakini pia hupunguza gharama, kwa kiasi kikubwa ikihakikisha ubora wa matunda hayo.
Katika miaka ya hivi karibuni, wilaya hiyo ya Yangbi imekuwa ikihamasisha maendeleo ya kilimo cha kidijitali, na kupanua zaidi njia za wakulima kuongeza mapato yao.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma