

Lugha Nyingine
Ushirikiano wa kilimo kati ya Gambia na China unazaa matokeo mazuri, asema waziri wa Gambia (5)
![]() |
Picha ya droni iliyopigwa Machi 13, 2025 ikionyesha shamba la mradi wa ushirikiano wa teknolojia ya kilimo wa China na Gambia katika Eneo la Kati la Mto, Gambia. (Xinhua/Si Yuan) |
BANJUL – Uungaji mkono na usaidizi wa kiufundi wa China umekuwa na jukumu muhimu katika kuchochoea maendeleo makubwa katika sekta ya kilimo nchini Gambia katika miaka ya hivi karibuni, Waziri wa Kilimo wa Gambia Demba Sabally ameliambia Shirika la Habari la China, Xinhua katika mahojiano maalum siku ya Jumatano wiki hii.
Tija ya kilimo ya Gambia imekuwa ikiongezeka kwa kasi, huku uzalishaji wa mpunga ukizidi tani 48,000 mwaka 2024, ikifikia kiwango cha juu katika kihistoria, Sabally amesema, akisisitiza kwamba ubunifu katika miundombinu na kuanzishwa kwa teknolojia ya kilimo chenye kutoa mavuno mengi na timu za China kumekuwa na mchango mkubwa katika kufikia hatua hiyo muhimu.
"Timu za kiufundi za China zimetoa usaidizi nchini Gambia kwa kuanzisha aina mbalimbali za mpunga wa ubora wa hali ya juu, ikiwa ni pamoja na mbegu zenye mavuno mengi na chotara, ambazo ni muhimu kwa maendeleo yetu ya kilimo," Sabally amesema.
Miaka ya hivi karibuni imeshuhudia ushirikiano wa teknolojia ya kilimo kati ya Gambia na China ukiongezeka kwa kiasi kikubwa. Tarehe 24 Februari 2023, awamu ya pili ya mradi wa ushirikiano wa teknolojia ya kilimo kati ya China na Gambia ilianza rasmi.
Hivi sasa, awamu ya pili ya mradi huo inaendelea vizuri, ikiwa na mafanikio makubwa katika kuwa kielelezo cha teknolojia ya mavuno mengi, uchaguaji na ukuzaji wa aina mbalimbali za mbegu, mafunzo ya kiufundi, na uungaji mkono wa miundombinu.
Mamlaka za Gambia zimepongeza sana mpango huo, hasa kwa michango yake kwa mbinu za kilimo cha mazao mengi, ufanyaji kilimo cha uzalishaji mpunga kuwa wa mashine, na uungaji mkono jumuiya za ushirika wa kilimo za wenyeji.
Sabally amesema kuwa wataalamu wa China wamesaidia kutatua changamoto mbalimbali katika sekta ya kilimo nchini Gambia.
"Katika awamu zote ya kwanza na ya pili ya ushirikiano, maafisa wengi wa kilimo wa Gambia walipelekwa China kwa mafunzo, wakati huohuo wataalam wa kilimo wa China wamekuwa wakitoa mwongozo wa kitaalamu kwa viongozi na wakulima wenyeji nchini Gambia," amesema.
"Shukrani kwa programu hizi za mafunzo, uzalishaji wetu wa kilimo umefikia hatua ya utayarishaji wa ardhi, upandaji na upandikizaji, uvunaji na usindikaji kwa kutumia mashine." ameongeza.
Sabally amewahi kutembelea China mara mbili kati ya 2023 na 2024, akivutiwa sana na ufanyaji wa kilimo cha kisasa na maendeleo ya mijini ya nchi hiyo.
"Pia tumefaidika sana kutokana na uzoefu wa maendeleo ya China. Miongo kadhaa iliyopita, hali ya uchumi wa China ilikuwa sawa na ya Gambia, lakini wamepata mafanikio makubwa wa kupiga hatua mbele kupitia mikakati fanisi ya maendeleo," amebainisha.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma