

Lugha Nyingine
Shughuli ya wiki ya kitamaduni yafanyika katika mji wa Nezha mjini Tianjin, China
(Tovuti ya Gazeti la Umma) Machi 18, 2025
![]() |
Watembeleaji wakichagua vitafunwa katika mji wa Nezha mjini Tianjin, kaskazini mwa China, Machi 16, 2025. (Xinhua/Sun Fanyue) |
Hivi karibuni, mji wa Nezha mjini Tianjin, kaskazini mwa China uliandaa shughuli ya wiki ya kitamaduni, ikihusisha shughuli mbalimbali zinazojikita katika maudhui ya Nezha, mhusika wa hekaya maarufu ya China na mambo mengine ya kijadi ya kitamaduni. Shughuli hiyo ilijumuisha maonyesho, gwaride changamani, na safari za usiku za taa za jadi, ikiwapa watembeleaji uzoefu wa kitamaduni wa kina.
Eneo la mji wa Nezha hapo awali eneo lilikuwa la Kiwanda cha Redio Bohai ya Tianjin, ambalo limefanyiwa mageuzi kama sehemu ya jitihada za Tianjin za ukarabati na ujenzi upya mjini. Eneo hilo lililohuishwa linajumuisha rasilimali zilizopo na mambo ya kijadi ya kitamaduni, likiingiza uhai mpya katika maendeleo bora ya hali ya juu ya uchumi wa eneo husika.
(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma