

Lugha Nyingine
Kijiji cha Kabila la Wadong la Zhaoxing, China: Kuperuzi mandhari ya desturi za kikabila katika majira ya mchipuko
Machi 17, katika majira ya mchipuko ya Kijiji cha Kabila la Wadong cha Zhaoxing, mashamba ya maua ya rapa yenye rangi ya dhahabu yalikuwa yamechanua sana. Katika kijiji hicho, nyimbo za kabila hilo la Wadong zilikuwa zikitamalaki hewani, na mashamba ya maua na nyimbo hizo kwa pamoja zimeunda picha za kuvutia.
Kijiji hicho kizuri cha Kabila la Wadong cha Zhaoxing kinapatikana katika Wilaya ya Liping ya Mkoa wa Guizhou, China. Kilijengwa 986 B.K. Kijiji hicho ni moja kati ya vijiji vikubwa zaidi vya kabila la Wadong nchini China, na kinajulikana kama “Kijiji Na. 1 kwenye maskani ya kabila la Wadong”.
Katika miaka ya hivi karibuni, kijiji hicho cha Zhaoxing kimekuwa kikiendeleza kwa bidii tasnia ya utalii kwa kutumia vizuri rasilimali yake ya utamaduni wa kabila la Wadong. Mwaka 2024, eneo la kivutio cha watalii la Zhaoxing lilipokea watalii zaidi ya milioni 1.02, na mapato jumuishi ya utalii yalikuwa Yuan bilioni 1.01. Wakati huohuo Kijiji hicho cha Zhaoxing kimekuwa kikitegemea ufundi wa jadi wa kazi za mikono wa kabila la Wadong kuanzisha bidhaa za kitamaduni na kibunifu, kama vile bidhaa za kudarizi za kabila la Wadong, hali ambayo imewezesha upatikanaji wa ajira na ujasiriamali kwa wanakijiji zaidi ya 2,000.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma