Shughuli ya "CIIE Yaingia Hubei" yafanyika Wuhan, China (6)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Machi 20, 2025
Shughuli ya

Shughuli ya "CIIE Yaingia Hubei" yenye kaulimbiu ya "Kuzidisha uagizaji na kuhudumia mizunguko ya uchumi" imefanyika mjini Wuhan, Mji Mkuu wa Mkoa wa Hubei, katikati mwa China Jumanne Machi, 18. CIIE ni kifupi cha Maonyesho ya Kimataifa ya Uagizaji Bidhaa ya China.

Shughuli hiyo iliratibiwa kwa pamoja na Wizara ya Biashara ya China na Serikali ya Mkoa wa Hubei na ni shughuli ya kwanza ya "CIIE Yaingia Miji na Wilaya" katika mwaka 2025.

Shughuli hiyo ilifanya matukio madogo kama vile mikutano ya uhamasishaji, mikutano maalum ya kutimiza mawasiliano kwa ajili ya sekta zenye faida, na ziara za utafiti.

Wakijikita katika tasnia muhimu za Hubei kama vile huduma ya afya, bidhaa za rejareja, utengenezaji magari na vifaa, waonyeshaji bidhaa 116 wa maonyesho ya CIIE, mashirika ya kukuza uwekezaji na kampuni za kimataifa zilialikwa kushiriki, ambapo 80 kati ya hizo ni miongoni mwa Kampuni Bora 500 duniani na viongozi wa tasnia.

Wadau zaidi ya 300 katika Mkoa wa Hubei wameshiriki katika ujenzi wa mitandao ya kibiashara, ikiwemo serikali za miji na maeneo husika, maeneo maalum ya viwanda, mamlaka husika za tasnia, kampuni maarufu za mkoa huo na wawakilishi wa jumuiya za wafanyabiashara.

Wakati wa ziara ya utafiti, Mkoa huo wa Hubei uliratibu waonyeshaji bidhaa na kampuni hizo za kimataifa kutembelea miji ya Wuhan, Xiangyang, Yichang na maeneo mengine kulingana na nia yao ya kupata miunganisho, ili kupata ufahamu wa kina wa mpangilio wa viwanda na kuchunguza fursa za ushirikiano.

Ili kuongeza ushawishi wa Maonyesho ya Kimataifa ya Uagizaji Bidhaa ya China (CIIE), ofisi ya Maonyesho hayo imeandaa mfululizo wa shughuli za "CIIE Yaingia Miji na Wilaya" tangu mwaka 2021, ili kuhimiza "vionyeshwa kuwa bidhaa, waonyeshaji kwa wawekezaji", kusaidia maendeleo ya uchumi wa maeneo husika, na kufikia matokeo mazuri.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha