Mawaziri wa uchumi na biashara wa China, Japan na Korea Kusini waahidi kuzidisha ushirikiano wa pande tatu

(Tovuti ya Gazeti la Umma) April 01, 2025
Mawaziri wa uchumi na biashara wa China, Japan na Korea Kusini waahidi kuzidisha ushirikiano wa pande tatu
Waziri wa Biashara wa China Wang Wentao akizungumza kwenye Mkutano wa 13 wa Mawaziri wa Uchumi na Biashara wa Pande Tatu za China-Japan- Korea Kusini mjini Seoul, Korea Kusini, Machi 30, 2025. (Xinhua/Yao Qilin)

SEOUL - China imedhamiria kwa maendeleo yenye sifa bora na kupanua ufunguaji mlango wa ngazi ya juu, ikiapa kunufaisha fursa na nchi zote, yakiwemo Korea Kusini(ROK) na Japan, amesema Waziri wa Biashara wa China Wang Wentao kwenye Mkutano wa 13 wa Mawaziri wa Uchumi na Biashara wa Pande Tatu za China-Japan- Korea Kusini uliofanyika Seoul Jumapili.

“Huku kukiwa na shinikizo kudidimia kwa uchumi duniani, China, Japan na Korea Kusini, zikiwa nchi zenye uchumi mkubwa katika kanda na duniani, zinapaswa kufanya juhudi za pamoja ili kulinda biashara huria na mfumo wa biashara wa pande nyingi, kupinga hatua za upande mmoja na kujihami kiuchumi, na kuendeleza mafungamano ya kiuchumi ya kikanda,” amesema Wang.

Mkutano huo wa pande tatu, uliojikita katika mada kama vile kuimarisha ushirikiano wa kibiashara na uwekezaji na kuendeleza ushirikiano wa kikanda na wa pande nyingi, uliongozwa kwa pamoja na Wang Wentao, Waziri wa Biashara, Viwanda na Nishati wa Korea Kusini Ahn Duk-geun, na Waziri wa Uchumi, Biashara na Viwanda wa Japan Yoji Muto.

Katika mkutano huo, idara za uchumi na biashara za nchi hizo tatu zimekubaliana kujadili kuharakisha mmazungumzo kuhusu makubaliano ya biashara huria ya pande tatu, kuimarisha ushirikiano wa mnyororo wa usambazaji wa bidhaa na mazungumzo kuhusu udhibiti wa mauzo ya nje, kuzidisha ushirikiano katika uchumi wa kidijitali na kijani, kuongeza ushirikiano wa serikali za mitaa, na kwa pamoja kujenga na kuhimiza mazingira mazuri kwa ushirikiano wa kibiashara.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha