

Lugha Nyingine
Maonyesho ya Mitindo ya Mavazi ya Kijiji yaunganisha utamaduni wa jadi na mitindo ya kisasa
GUIYANG - Kwenye jukwaa la mbao la wanamitindo kutembelea lililojengwa kwenye mashamba ya matuta ya mteremko milimani ya Jiabang Mkoa wa Guizhou, kusini-magharibi mwa China, wanakijiji wa kabila la Wamiao, wakiwa wamevalia mavazi yao ya kifahari, wamejitokeza katika maonyesho hayo ya mitindo ya mavazi lenye kauli mbiu ya urithi wa utamaduni usioshikika.
Mapambo ya madini ya fedha yakining'inia kwenye nywele zao, huku baadhi ya wanakijiji wakiwa wamebeba zana za kilimo kama vile majembe na plau, na vikapu vilivyojaa bata na samaki, kwa ufahari wakionyesha mila za kilimo ambazo zimepitishwa kwa maelfu ya miaka.
Mashamba hayo ya matuta ya mteremko milimani yametumika kama mandhari ya wanamitindo waliovalia nguo zilizopambwa kwa darizi, batiki na mapambo ya madini ya fedha ya kabila la Wamiao, walipokuwa wakitembea kwenye jukwaa. Roboti na Roboti mbwa, katika mapambo ya Wamiao, pia zilishiriki katika maonyesho hayo.
Stephen Jones, mtalii wa Australia ambaye alikuwa akitembelea China kwa mara ya tano, ametumia simu yake janja kunasa shughuli hiyo, akipongeza mara kwa mara maonyesho hayo ya mitindo, pamoja na mandhari ya milimani na mashamba ya mpunga yaliyo karibu.
"Ikilinganishwa na Australia, China ina historia ya maelfu ya miaka na tamaduni tajiri za makabila madogo. Ni mara yangu ya kwanza kutembelea mashamba ya matuta ya mteremko milimani ya Jiabang, ambayo inaniletea hali ya kusafiri isiyo na kifani, hasa sherehe za shughuli hizo za kilimo na desturi za makabila madogo ya wenyeji," Jones amesema.
"Ni vizuri kupata uzoefu na kushuhudia shughuli hizi za sherehe. Ni safari isiyoweza kusahaulika kwangu." ameongeza.
Mwanablogu Mjerumani Robert Adolf, ambaye alikuwa akirekodi tukio hilo, alisogea karibu na jukwaa kwa furaha. Kabla ya kuanzisha kwa maonyesho hayo, alirekodi video fupi kwa Kijerumani, akitambulisha uzuri wa mazingira ya asili wa mashamba hayo ya Jiabang huku akirekodi uzoefu wake wa kwanza wa kushiriki kwenye maonyesho hayo ya mitindo ya mavazi katika eneo hilo.
"Kuchagua eneo hili kufanya maonyesho ni ya maalum na mazuri. Pamoja na mambo ya kijadi ya kitamaduni yakiunganishwa na maonyesho ya kisasa, hii ni njia nzuri ya kuonyesha dunia utamaduni mzuri wa watu wa kabila la Wamiao," Adolf amesema.
"Juni ijayo, maonyesho ya mitindo ya mavazi ya kijiji ya Guizhou yitapeleka urithi wa utamaduni usioshikika wa China kwenye Maonyesho ya Dunia ya 2025 mjini Osaka nchini Japan, na hivyo kuwasilisha maonyesho hayo ya mitindo ya mavazi ya urithi wa utamaduni usioshikika kwenye jukwaa pana la kimataifa," amesema Gao Changjiang, mkurugenzi mtendaji wa maonyesho hayo.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma