China kushughulikia usafiri wa abiria milioni 144 kwenye njia za reli wakati wa likizo ya Mei Mosi (3)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) April 30, 2025
China kushughulikia usafiri wa abiria milioni 144 kwenye njia za reli wakati wa likizo ya Mei Mosi
Abiria wakisubiri kupanda treni katika Stesheni ya Reli ya Tengzhou Mashariki mjini Tengzhou, Mkoa wa Shandong, mashariki mwa China, Aprili 29, 2025. (Picha na Li Zongxian/Xinhua)

BEIJING – Kampuni kuu ya Reli ya China imesema, mtandao wa reli ya China unatarajiwa kushughulikia usafiri wa abiria milioni 144 katika siku nane kuanzia jana, ambazo ni kipindi cha pilika za wasafiri wengi za likizo ya Siku ya Wafanyakazi Duniani, Mei Mosi. Takwimu hizo zimeonesha kuwa ongezeko la usafiri wa watu wa kipindi hicho litafikia asilimia 4.9 kuliko mwaka jana.

Alhamisi inatarajiwa kushuhudia kilele cha usafiri wa abiria wengi katika siku hizo za mapumziko, kampuni hiyo ya reli ya kitaifa imesema.

Kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa kwenye jukwaa la 12306 la China la kuweka oda za tiketi za usafiri wa reli, sehemu maarufu kwa watu kutembelea katika likizo hiyo ni pamoja na miji ya Beijing, Shanghai, Guangzhou, Chengdu, Hangzhou, Wuhan, Shenzhen, Xi'an, Nanjing na Zhengzhou.

Takwimu za jukwaa hilo pia zinaonyesha kuwa njia za reli za Beijing-Shanghai, Xi'an-Chengdu, Beijing-Hohhot, Nanning-Guangzhou, Beijing-Shenyang, na Shenzhen-Hong Kong ni njia zitakazokuwa na wasafiri wengi zaidi katika siku nane hizo za mapumziko.

Ili kukidhi mahitaji ya ongezeko hilo la wasafiri, mamlaka za reli za China zimepanga huduma za ziada za treni. Kwa wastani, treni za abiria zaidi ya 12,000 zinafanya usafiri kila siku, kampuni hiyo imesema.

Kampuni hiyo imesema kuwa hatua kama vile kupanga kwenye ratiba treni za ziada za mwendokasi za watu kulala ndani yake usiku zimechukuliwa ili kuongeza uwezo wa usafiri katika sehemu zenye wasafiri wengi na nyakati za pilika za wasafiri wengi. 

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha