

Lugha Nyingine
Ikulu ya White House yasema mpango wa Amazon kuonyesha gharama za ushuru ni "uhasama na hatua ya kisiasa" (2)
WASHINGTON - Ikulu ya White House imekosoa uamuzi wa kampuni kubwa ya kuuza bidhaa ya Amazon wa kuonyesha gharama za ushuru pamoja na bei ya bidhaa zake ambapo akijibu kuhusu habari juu ya hatua hiyo ya pangwa ya Amazon, Msemaji wa Ikulu ya White House Karoline Leavitt Jumanne ameiita uamuzi huo kuwa ni "uhasama na hatua ya kisiasa."
Amesema hayo kwenye mkutano na waandishi wa habari pamoja na Waziri wa Hazina wa Marekani, Scott Bessent.
"Kwa nini Amazon haikufanya hivyo wakati utawala wa Biden ulipopandisha mfumuko wa bei hadi kiwango cha juu zaidi katika miaka 40 iliyopita?" Leavitt amehoji, akihimiza Wamarekani "kununua bidhaa za Marekani."
Mapema jana Jumanne, chombo cha habari cha Punchbowl News kiliripoti kwamba Amazon inakusudia kuonyesha gharama za ushuru zilizowekwa chini ya utawala wa Rais Donald Trump kama sehemu ya bei ya kila bidhaa.
"Amazon haitaki kubeba lawama kwa gharama ya vita vya biashara vya Rais Donald Trump. Kwa hivyo kampuni kubwa ya biashara ya mtandaoni itaonyesha hivi karibuni ni kiasi gani ushuru wa Trump unaongeza bei ya kila bidhaa," habari hiyo iliyoripotiwa inasema, ikinukuu chanzo chenye ufahamu wa mpango huo.
Wafanyabiashara wengi wa kuuza bidhaa kwa bei za reja reja wameelezea wasiwasi kuhusu gharama za ziada zinazotokana na ushuru. Katika ripoti ya mapema mwezi huu, watendaji wa Best Buy walisema ushuru huo mpya "unaweza kuongeza gharama, kuvuruga mnyororo wetu wa uzalishaji na/au kuathiri upatikanaji wa teknolojia ya msingi ambazo ni muhimu kwa shughuli zetu."
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma