

Lugha Nyingine
Shirikisho la Wafanyabiashara wa China barani Afrika laanzishwa ili kukuza ushirikiano mpana kati ya China na Afrika (3)
![]() |
Moussa Mohamed Omar, naibu mkuu wa wafanyakazi wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika, akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa Shirikisho la Wafanyabiashara wa China barani Afrika mjini Addis Ababa, Ethiopia, Aprili 28, 2025. (Xinhua/Michael Tewelde) |
ADDIS ABABA – Shirikisho la Wafanyabiashara wa China barani Afrika (CCCA) limezinduliwa rasmi juzi Jumatatu katika mji mkuu wa Ethiopia, Addis Ababa, kwa lengo la kukuza ushirikiano mpana kati ya China na Afrika na kutoa mchango kwa ajili ya jumuiya ya karibu zaidi ya China na Afrika yenye mustakabali wa pamoja.
Likijumuisha wanachama 15 waanzilishi, CCCA linahusisha sekta mbalimbali, zikiwemo za kilimo, ujenzi, viwanda, mawasiliano ya simu, nishati, na afya. Huku wanachama wakitarajiwa kuongezeka katika shughuli za jadi na zinazoibukia, shirikisho hilo linalenga kuimarisha uhusiano wa kiuchumi na kuwezesha ushirikiano wa kiuchumi kati ya China na Afrika.
Akihutubia hafla ya uzinduzi wa shirikisho hilo, Mkuu wa Ujumbe wa China kwenye Umoja wa Afrika (AU), Hu Changchun, amesema shirikisho hilo lililozinduliwa, chini ya mwongozo wa ujumbe huo, litatumika kama daraja la kuhimiza China, Afrika na jumuiya pana ya Nchi za Kusini kupata maendeleo kwa pamoja.
"Kuanzishwa kwa shirikisho hili kutaleta mapatano bora zaidi kwa ushirikiano wa kiuchumi kati ya China na Afrika, na kuwezesha urafiki wetu kuimarika zaidi. Ninatumai kwa dhati kuwa shirikisho hili litaleta wanachama wengi zaidi, litashirikiana na wadau wote, na kutoa mchango katika kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara kati ya China na Afrika," amesema Hu.
Kwa mujibu wa takwimu za ujumbe wa China kwenye Umoja wa Afrika, kampuni za China zimekuwa zikitoa mchango kwa muda mrefu maendeleo ya Afrika, zikijenga takriban kilomita 100,000 za barabara, kilomita 10,000 za reli, madaraja 1,000 na bandari 100, huku zikitoa ajira zaidi ya milioni 1 katika bara zima. Juhudi hizo zimeboresha kwa kiasi kikubwa muunganisho wa uchukuzi, ujumuishaji wa minyororo ya thamani ya kikanda, na maisha ya watu katika bara la Afrika.
Moussa Mohamed Omar, naibu mkuu wa wafanyakazi wa Kamisheni ya AU, amesema kuanzishwa kwa CCCA chini ya ushirikiano wa kimkakati kati ya China na Afrika inaonyesha ushirikiano wa kunufaishana unaojengwa juu ya msingi wa kuheshimiana na ushirikiano wenye matokeo halisi.
Akibainisha kuwa kampuni za China zinajishughulisha kikamilifu na sekta mbalimbali za maendeleo barani Afrika, zikiwemo sekta za miundombinu, nishati, miundombinu ya kidijitali na usambazaji, Omar amesema kampuni za China zinatoa mchango mkubwa maendeleo ya Afrika na utoaji wa ajira.
Wu Jiuyi, katibu mkuu wa CCCA ambaye pia ni naibu meneja mkuu wa Shirika la Ujenzi wa Uhandisi wa Miundombinu la China Tawi la Ethiopia, amesema shirikisho hilo limekita mizizi barani Afrika ili kuhudumia kampuni, kukuza ushirikiano, na kuhimiza kustawisha kwa pamoja.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma