Maonyesho ya 137 ya Canton yamalizika kwa rekodi ya idadi ya wanunuzi wa ng'ambo (7)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Mei 06, 2025
Maonyesho ya 137 ya Canton yamalizika kwa rekodi ya idadi ya wanunuzi wa ng'ambo
Wanunuzi wakizungumza na mwonyeshaji bidhaa kwenye banda la mavazi katika Maonyesho ya 137 ya Uagizaji na Uuzaji Bidhaa Nje ya China mjini Guangzhou, Mkoa wa Guangdong kusini mwa China, Mei 5, 2025. (Xinhua/Huang Guobao)

GUANGZHOU - Maonyesho ya 137 ya Uagizaji na Uuzaji Bidhaa Nje ya China, ambayo pia yanajulikana kwa jina la Maonyesho ya Canton, yamefungwa jana Jumatatu katika Mkoa wa Guangdong kusini mwa China, huku waandaaji wakitangaza ushiriki wa wanunuzi zaidi ya 288,000 wa ng'ambo.

Waandaaji walisema, idadi hiyo ni ongezeko la asilimia 17.3 kuliko maonyesho yaliyopita na kufikia rekodi mpya. Waandaaji wameeleza kuwa, kulikuwa na washiriki 171,750 kwa mara ya kwanza huku wanunuzi kutoka nchi zinazoshiriki katika ushirikiano wa Ukanda Mmoja, Njia Moja wakifikia 187,450, ongezeko la asilimia 17.4 kuliko ile ya maonesho yaliyopita na wakichukua asilimia 64.9 ya wanunuzi wote wa ng'ambo.

“Maonesho hayo yalivutia wanunuzi zaidi ya 527,000 mtandaoni kutoka nchi na maeneo 229 duniani” waandaaji wamesema.

Aidha, wameeleza kuwa, jumla ya vitu milioni 4.55 vimeonyeshwa, zikiwemo bidhaa mpya milioni 1.02, bidhaa 880,000 za kijani na zenye kutoa kaboni chache, na bidhaa za teknolojia za kisasa 320,000.

Waandaaji pia wameeleza kuwa, eneo la maonesho ya kwanza ya roboti za huduma yamekuwa kivutio cha maonyesho hayo, ambapo wafanyabiashara 46 wa roboti wa China wakiwasilisha zaidi ya roboti 500 za teknolojia ya hali ya juu zinazoshughulikia matumizi 60 ya kiviwanda.

Yakiwa yalianzishwa rasmi mwaka 1957, Maonyesho ya Canton hufanyika mara mbili kwa mwaka katika Mji wa Guangzhou. Hizi ni shughuli za muda mrefu zaidi za biashara na huduma za aina mbalimbali za kimataifa nchini China na zimekuwa zikisifiwa kama kipimo cha biashara ya nje ya China.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha