Israel yaonya mashambulizi makali dhidi ya Gaza, huku afisa mwandamizi akisema dirisha bado liko wazi kwa makubaliano (3)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Mei 06, 2025
Israel yaonya mashambulizi makali dhidi ya Gaza, huku afisa mwandamizi akisema dirisha bado liko wazi kwa makubaliano
Wapalestina wakitafuta manusura baada ya mashambulizi ya Israel katika kambi ya wakimbizi ya Jabalia, kaskazini mwa Ukanda wa Gaza, Mei 2, 2025. (Picha na Rizek Abdeljawad/Xinhua)

JERUSALEM/GAZA-Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu ameonya Jumatatu kwamba mashambulizi mapya ya nchi hiyo katika Ukanda wa Gaza yatakuwa "makali," akirejelea mpango ulioidhinishwa na baraza lake la mawaziri la usalama wakati wa usiku juu ya kuzidisha opresheni inayoendelea mjini Gaza ambapo chini ya mpango huo Israeli itapanua mashambulizi ya kutwaa Gaza, kudhibiti misaada, na kuhamisha wakazi kusini mwa ukanda huo.

"Tuko katika kipindi cha kuelekea uvamizi mkali ndani ya Gaza," Netanyahu amesema katika ujumbe wa video uliochapishwa kwenye mtandao wa kijamii wa X, akiongeza kuwa malengo ya operesheni hiyo ni "kuishinda Hamas na, katika mchakato huo, kuhakikisha kuachiliwa kwa mateka."

Amesema kuwa chini ya mpango huo, Israel itabadilisha mkakati wake wa sasa, kusonga mbele kutoka kujiondoa baada ya kuharibu uwezo wa kijeshi wa Hamas hadi kudumisha udhibiti wa eneo lililotekwa la Gaza.

Siku ya Jumatatu, Hamas ililaani mpango huo mpya wa usambazaji misaada wa Israeli kama "hila ya kisiasa." Katika taarifa kwa vyombo vya habari, Hamas imesema kuwa mpango huo utabadilisha misaada ya kibinadamu kuwa chombo cha kisiasa, kukiuka sheria za kimataifa, na kusababisha "njaa na kulazimishwa kuhama makazi" katika ukanda wa pwani.

Raundi kadhaa za mazungumzo ya upatanishi zimeshafanyika hivi karibuni, lakini zote zimeshindwa kurejesha usimamishaji vita mjini Gaza kutokana na tofauti kati ya pande hizo.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha