Naibu Waziri Mkuu wa China akutana na mwenyekiti wa kamati ya usimamizi ya Mamlaka ya Uwekezaji ya Abu Dhabi (2)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Mei 08, 2025
Naibu Waziri Mkuu wa China akutana na mwenyekiti wa kamati ya usimamizi ya Mamlaka ya Uwekezaji ya Abu Dhabi
Naibu Waziri Mkuu wa China He Lifeng, ambaye pia ni Mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China, akikutana na Majed Al Romaithi, mwenyekiti wa Kamati ya Usimamizi ya Mamlaka ya Uwekezaji ya Abu Dhabi (ADIA) ya Umoja wa Falme za Kiarabu, mjini Beijing, mji mkuu wa China, Mei 7, 2025. (Xinhua/Yue Yuewei)

BEIJING – Naibu Waziri Mkuu wa China He Lifeng amekutana na Majed Al Romaithi, mwenyekiti wa Kamati ya Usimamizi ya Mamlaka ya Uwekezaji ya Abu Dhabi (ADIA) ya Umoja wa Falme za Kiarabu, mjini Beijing jana Jumatano akisema kuwa uchumi wa China umeanza vyema mwaka huu, huku maendeleo bora ya kiwango cha juu yakisonga mbele na imani na matarajio ya kijamii zimeendelea kuboreshwa.

"China inaendelea kuzidisha mageuzi yake kwa pande zote, na ikifanya jitihada za kuhimiza ufunguaji mlango wa ngazi ya juu katika nyanja mbalimbali kama vile mambo ya fedha" He, ambaye pia ni mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) amebainisha, akiongeza kuwa China inakaribisha taasisi za fedha za kigeni ikiwemo ADIA na wawekezaji wa muda mrefu kufanya biashara nchini China na kunufaisha kwa pamoja fursa za maendeleo ya China.

Kwa upande wake Majed amesema ADIA ina matumaini kuhusu mustakabali wa uchumi wa China na inatazamia kufanya ushirikiano na mawasiliano na China katika sekta mbalimbali.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha