

Lugha Nyingine
Marais wa China na Russia wakutana na wanahabari baada ya mazungumzo
Rais Xi Jinping wa China na mwenzake wa Russia Vladimir Putin wamefanya mkutano na wanahabari baada ya kufanya mazungumzo Ikulu ya Russia jana Alhamisi, Mei 18.
Kwenye mkutano huo, Rais Xi amesema katika mazungumzo yake na Rais Putin wamefikia makubaliano mengi mapya muhimu, ambapo wamesaini “Taarifa ya pamoja juu ya kuimarisha zaidi Ushirikiano wa Washirika wa Kimkakati wa Uratibu wa Pande zote kati ya China na Russia katika zama mpya”, na kuingiza nguvu mpya katika maendeleo ya uhusiano kati ya China na Russia.
Rais Xi amesisitiza kuwa katika kukabiliana na mabadiliko ya dunia, zama na historia, China na Russia zinapaswa kutoa mchango mpya mkubwa zaidi katika kuhimiza maendeleo na ustawi wa nchi hizo mbili na kulinda haki na usawa wa kimataifa.
Amesema, China na Russia zinapaswa kushikilia urafiki unaoendelea kizazi baada ya kizazi, kushikilia kunufaishana, usawa na haki, na kufanya kazi pamoja.
Ameongeza kuwa katika kukabiliana na hali ya kimataifa yenye mabadiliko na sintofahamu, China na Russia zinapaswa kudumisha ujirani mwema, kuimarisha uratibu wa kimkakati, kuongeza ushirikiano wa kunufaishana, na kuinua kiwango, wigo na uhimilivu wa uhusiano kati ya China na Russia kwa pande zote, ili kuleta utulivu zaidi kwenye amani na usalama wa dunia, na kutoa msukumo zaidi kwa maendeleo na ustawi wa dunia.
Upandaji mahindi waingia kipindi cha kilele katika Mkoa wa Mongolia ya Ndani, China
UNESCO latoa wito upya wa kuimarishwa ulinzi wa maeneo ya urithi ya Afrika
Maonyesho ya Kimataifa ya Baiskeli ya China 2025 yaanza Shanghai
Shaolin Kungfu, chombo muhimu cha mawasiliano ya Utamaduni wa China na ulimwengu wa nje
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma