

Lugha Nyingine
China yaitaka Marekani kuonyesha udhati katika mkutano ujao wa ngazi ya juu kuhusu uchumi na biashara
BEIJING - Msemaji wa Wizara ya Biashara ya China He Yadong kwenye mkutano na waandishi wa habari jana Alhamisi ametoa wito kwa Marekani kuonyesha udhati kama upande wa Marekani unataka kutatua mzozo wa kibiashara kati ya nchi hizo mbili kupitia majadiliano.
He amesema, China imekuwa ikidumisha siku zote msimamo thabiti dhidi ya matumizi mabaya ya hatua za ushuru ya Marekani, akihimiza upande wa Marekani kufuatilia zaidi athari hasi mbaya kwa nchi yake yenyewe na jumuiya ya kimataifa kutokana na hatua zake za upande mmoja za kutoza kodi ya juu.
"Upande wa Marekani unapaswa kufanya maandalizi na kuchukua hatua za kurekebisha vitendo vyake potofu na kuondoa hatua za kutoza kodi ya juu za upande wake mmoja," msemaji huyo amesema wakati akijibu swali la mwandishi wa habari kuhusu mkutano ujao wa ngazi ya juu wa uchumi na biashara kati ya nchi mbili China na Marekani.
Msemaji huyo ameutaka upande wa Marekani kuheshimu sheria za kimataifa za uchumi na biashara, kushikilia haki na usawa, kusikiliza sauti zenye mantiki kutoka watu wa sekta mbalimbali, na kuonyesha udhati katika mazungumzo.
"Tunatumai upande wa Marekani utafanya juhudi na China kwa mwelekeo sawasawa na kushughulikia masuala ya pande zote mbili kwa mashauriano ya usawa," msemaji huyo amesema.
"Lakini kama Marekani itasema jambo moja huku ikifanya jambo lingine, au hata kujaribu kuendelea kulazimisha na kulaghai chini ya kivuli cha mazungumzo, China haitakubali kamwe, wala haitataka kufikia makubaliano yoyote kwa kutoa kafara kanuni na msimamo wake vilevile haki na usawa wa kimataifa," amesema.
Wizara ya Mambo ya Nje ya China ilitangaza Jumatano kwamba He Lifeng, mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China ambaye pia ni Naibu Waziri Mkuu wa Baraza la Serikali la China, atafanya ziara Uswisi kuanzia Mei 9 hadi 12. Katika ziara yake hiyo, He, atakuwa kiongozi wa upande wa China kuhusu mambo ya uchumi na biashara na Marekani, na atafanya mkutano na Waziri wa Fedha wa Marekani Scott Bessent, ambaye ni kiongozi wa upande wa Marekani kuhusu mambo hayo.
Upandaji mahindi waingia kipindi cha kilele katika Mkoa wa Mongolia ya Ndani, China
UNESCO latoa wito upya wa kuimarishwa ulinzi wa maeneo ya urithi ya Afrika
Maonyesho ya Kimataifa ya Baiskeli ya China 2025 yaanza Shanghai
Shaolin Kungfu, chombo muhimu cha mawasiliano ya Utamaduni wa China na ulimwengu wa nje
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma