Naibu Waziri Mkuu wa China asema mkutano na Marekani umekuwa wa kina, wa wazi na wa kiujenzi

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Mei 12, 2025

Mkutano na waandishi wa habari ukifanywa na upande wa China kufuatia Mkutano wa Nganzi ya Juu kati ya China na Marekani juu ya masuala ya kiuchumi na biashara mjini Geneva, Uswisi, tarehe 11 Mei 2025. (Xinhua/Zhao Dingzhe)

Mkutano na waandishi wa habari ukifanywa na upande wa China kufuatia Mkutano wa Nganzi ya Juu kati ya China na Marekani juu ya masuala ya kiuchumi na biashara mjini Geneva, Uswisi, tarehe 11 Mei 2025. (Xinhua/Zhao Dingzhe)

GENEVA – Naibu Waziri Mkuu wa China He Lifeng amesema mjini Geneva, Uswisi jana Jumapili kwamba mkutano wa ngazi ya juu kuhusu masuala ya kiuchumi na biashara kati ya China na Marekani umekuwa wa kina, wa wazi na wa kiujenzi.

He, kiongozi wa ujumbe wa China kwa masuala ya kiuchumi na biashara kati ya China na Marekani, amesema hayo alipokuwa akitoa taarifa kwa waandishi wa habari baada ya mkutano huo.

Afisa huyo mwandamizi wa China amesema pande hizo mbili zimefikia maafikiano kadhaa muhimu, akiongeza kuwa China na Marekani pia zimekubaliana kuanzisha utaratibu wa mashauriano ya kiuchumi na kibiashara.

He amesema, China na Marekani zitakamilisha mambo halisi husika haraka iwezekanavyo na kwamba zitatoa leo Jumatatu taarifa ya pamoja iliyofikiwa katika mazungumzo hayo.

Amefahamisha kuwa kutokana na hali ilivyo sasa mkutano huo umekuwa ukifuatiliwa kwa karibu na jumuiya ya kimataifa.

“Kupitia juhudi za pamoja za pande zote mbili, mazungumzo hayo yamezaa matunda,” amesema He, akiongeza kuwa ni hatua muhimu ya kusuluhisha tofauti kupitia njia ya mazungumzo na mashauriano kwa usawa, na imeweka msingi na kuweka mazingira ya kupunguza zaidi tofauti na kuzidisha ushirikiano.

Amesema, uhusiano wa kiuchumi na kibiashara kati ya China na Marekani si tu kwamba una umuhimu mkubwa kwa nchi hizo mbili bali pia una athari kubwa katika utulivu na maendeleo ya uchumi wa dunia.

“China ingependa kushirikiana na Marekani kutekeleza kikamilifu makubaliano yaliyofikiwa na wakuu wawili wa nchi hizo kwenye mazungumzo yao ya simu Januari 17,” ameongeza.

Pia ametoa wito kwa pande hizo mbili kufuata mtazamo wa kivitendo wa kutatua matatizo, kufanya mazungumzo ya wazi na mashauriano sawa, kudhibiti tofauti, kuchunguza uwezekano wa ushirikiano, kupanua orodha ya mambo ya ushirikiano, na kupanua zaidi ushirikiano, ili kusukuma maendeleo mapya ya uhusiano wa kiuchumi na kibiashara kati ya China na Marekani, na kuingiza uhakika na utulivu zaidi katika uchumi wa dunia.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha