

Lugha Nyingine
Huawei yatambulisha mfumo wa AI unaowezeshwa na teknolojia ya wingu kuunga mkono elimu nchini Zambia
Kampuni ya teknolojia ya mawasiliano ya China, Huawei, imetangaza mwishoni mwa wiki iliyopita kuanzisha teknolojia ya Akili Mnemba (AI) inayowezeshwa na teknolojia wingu kwa nchi ya Zambia ili kuunga mkono upatikanaji wa uhakika wa elimu katika maeneo yasiyo na mtandao.
Katibu Mkuu anayehusika na utawala katika Wizara ya Elimu ya Zambia Noriana Muneku ameishukuru Huawei kwa kuwa mfano mzuri wa washirika wa kidijitali nchini humo kwa zaidi ya miaka 20.
Amesema serikali inatarajia kuendeleza mageuzi ya sekta ya elimu kupitia ushirikiano na kampuni hiyo.
Makamu Rais wa Huawei katika kanda ya Afrika kusini mwa Jangwa la Sahara, Lei Yang, amesema teknolojia hiyo itawezesha wanafunzi katika maeneo ya vijijini kupata elimu ya kisasa.
Ameongeza kuwa, licha ya kuanzisha mazingira mazuri zaidi ya kujifunza, mfumo huo unaweza kuunga mkono tafsiri ya lugha na urahisishaji wa mtaala wa masomo.
Upandaji mahindi waingia kipindi cha kilele katika Mkoa wa Mongolia ya Ndani, China
UNESCO latoa wito upya wa kuimarishwa ulinzi wa maeneo ya urithi ya Afrika
Maonyesho ya Kimataifa ya Baiskeli ya China 2025 yaanza Shanghai
Shaolin Kungfu, chombo muhimu cha mawasiliano ya Utamaduni wa China na ulimwengu wa nje
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma