

Lugha Nyingine
Upinzani nchini Sudan Kusini wadai kushikilia maeneo ya mpakani
Chama cha upinzani cha SPLM-IO cha nchini Sudan Kusini kinachoongozwa na Makamu wa Kwanza wa Rais wa nchi hiyo, Riek Machar, kimedai kuwa kimedhibiti tena miji kadhaa karibu na mipaka ya Sudan Kusini na Uganda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).
Msemaji wa SPLM-IO Lam Paul Gabriel amesema katika taarifa iliyotolewa Juba, juzi Jumamosi, kwamba wamedhibiti maeneo ya Kendila, Panyume, Mongoya na Lujulo katika Jimbo la Ikweta ya Kati siku ya Alhamis baada ya mapambano kati yake na Jeshi la Ulinzi la Sudan Kusini na Vikosi vya Usalama wa Taifa.
Mapigano kati ya pande hizo mbili yameongezeka tangu tarehe 26 Machi mwaka huu katika maeneo mbalimbali ya Sudan Kusini, hususan katika majimbo ya Upper Nile, Unity na Ikweta ya Kati.
Upandaji mahindi waingia kipindi cha kilele katika Mkoa wa Mongolia ya Ndani, China
UNESCO latoa wito upya wa kuimarishwa ulinzi wa maeneo ya urithi ya Afrika
Maonyesho ya Kimataifa ya Baiskeli ya China 2025 yaanza Shanghai
Shaolin Kungfu, chombo muhimu cha mawasiliano ya Utamaduni wa China na ulimwengu wa nje
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma