

Lugha Nyingine
Mradi wa awamu ya pili ya Bandari ya Kribi nchini Cameroon iliyojengwa na Kampuni ya China waanza kazi rasmi
Hafla ya uzinduzi rasmi ya awamu ya pili ya mradi wa Bandari ya Kribi nchini Cameroon ambayo imejengwa na Kampuni ya Ujenzi wa Bandari ya China imefanyika hivi karibuni katika bandari hiyo.
Katika hafla hiyo, Waziri wa Uchukuzi wa Cameroon Jean Ernest Massena Ngalle Bibehe amesema, uendeshaji wa mradi huo ni mwanzo mpya wa ukuaji wa uchumi wa nchi hiyo, na utachangia katika mageuzi ya muundo wa kiuchumi wa nchi hiyo.
Meneja Mkuu wa Kituo cha Usimamizi cha kampuni hiyo katika eneo la katikati ya Afrika Chen Ze ameeleza kuwa, kampuni hiyo ina imani kubwa juu ya uendeshaji wa mradi huo na maendeleo endelevu ya nchi hiyo.
Upandaji mahindi waingia kipindi cha kilele katika Mkoa wa Mongolia ya Ndani, China
UNESCO latoa wito upya wa kuimarishwa ulinzi wa maeneo ya urithi ya Afrika
Maonyesho ya Kimataifa ya Baiskeli ya China 2025 yaanza Shanghai
Shaolin Kungfu, chombo muhimu cha mawasiliano ya Utamaduni wa China na ulimwengu wa nje
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma