

Lugha Nyingine
Watu 62 wafariki kutokana na mafuriko mashariki mwa DRC
Watu 62 wamefariki kufuatia mafuriko yaliyokumba eneo la Fizi katika Jimbo la Kivu Kusini, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) usiku wa kuamkia Ijumaa hadi Jumamosi.
Mpaka sasa, mvua kubwa imesababisha mafuriko katika eneo la Kasaba, na kubomoa nyumba 150, kujeruhi watu 30, na wengine kadhaa bado hawajulikani walipo.
Serikali ya jimbo hilo imeeleza wasiwasi mkubwa juu ya kuongezeka kwa hatari ya magonjwa yatokanayo na maji, yakiwemo ya mfumo wa upumuaji na utapiamlo, kutokana na mvua hizo.
Majimbo mengine mengi likiwemo la Tanganyika pia yanakabiliwa na mafuriko yanayotokea mara kwa mara kutokana na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha.
Upandaji mahindi waingia kipindi cha kilele katika Mkoa wa Mongolia ya Ndani, China
UNESCO latoa wito upya wa kuimarishwa ulinzi wa maeneo ya urithi ya Afrika
Maonyesho ya Kimataifa ya Baiskeli ya China 2025 yaanza Shanghai
Shaolin Kungfu, chombo muhimu cha mawasiliano ya Utamaduni wa China na ulimwengu wa nje
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma