Msemaji: Ziara ya Rais wa Brazil nchini China ina umuhimu mkubwa

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Mei 13, 2025

BEIJING - Ziara ya Rais wa Brazil Luiz Inacio Lula da Silva nchini China ina umuhimu mkubwa katika hali ya hivi sasa ya kimataifa yenye mabadiliko na misukosuko, msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Lin Jian amesema Jumatatu.

Akisema kuwa China na Brazil zote ni nchi kubwa zinazoendelea, nchi zenye masoko makubwa yanayoibukia na nchi wanachama muhimu wa BRICS na Nchi za Kusini, Lin amesema uhusiano kati ya China na Brazil siku zote umekuwa safu ya mbele ya uhusiano wa China na nchi zinazoendelea.

Amesema, kutokana na mwaliko wa Rais Xi Jinping wa China, Rais Lula anafanya ziara ya kiserikali nchini China kuanzia Mei 10 hadi 14.

Lin amesema kuwa, China na Brazil ziliadhimisha miaka 50 tangu kuanzishwa uhusiano wa kidiplomasia mwaka jana.

Amesema, “Wakati wa ziara yenye mafanikio ya Rais Xi mwaka 2024 nchini Brazil, wakuu hao wawili wa nchi kwa pamoja walitangaza kuinua uhusiano wa pande mbili hadi jumuiya ya China na Brazil yenye mustakabali wa pamoja, ambapo zitajikita katika kujenga dunia yenye haki zaidi na sayari ya dunia yenye uendelevu zaidi, na kuanzishwa kwa ushirikiano chini ya Pendekezo la Ukanda Mmoja, Njia Mojaa na mikakati ya maendeleo ya Brazil,” na uhusiano wa pande mbili umeingia katika kipindi kipya cha kihistoria.

Msemaji huyo amesema, "Rais Lula ni kiongozi wa nchi kubwa ya Latin Amerika na mwanasiasa mwandamizi wa kimataifa mwenye ushawishi mkubwa," na hii ni ziara ya sita ya Lula nchini China, na ni ya pili kwake tokea mwaka 2023.

Lin amesema, ziara hiyo itaongeza zaidi mambo ya kimkakati ya jumuiya ya China na Brazil yenye mustakabali wa pamoja, na kuonyesha dhamira na wajibu thabiti wa China na Brazil wa kuongoza Nchi za Kusini katika kuimarisha mshikamano na ushirikiano na kuhimiza utulivu na ustawi wa kikanda na dunia.

Ameongeza kuwa, katika ziara yake hiyo, Rais Lula atahudhuria kwenye ufunguzi wa mkutano wa nne wa mawaziri wa Jukwaa kati ya China na CELAC (Jumuiya ya Nchi za Latin Amerika na Caribbean).

“China itatilia maanani sana kwa umuhimu wa Brazil katika mambo ya Latin Amerika na Caribbean (LAC) na inapenda kushirikiana na Brazil katika kuhimiza maendeleo mapya katika ujenzi wa jumuiya ya China na LAC yenye mustakabali wa pamoja,” amesema. 

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha