China yaingia zama ya 5G-A

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Mei 13, 2025

China inaharakisha ufungaji wa mitandao ya 5G- ya hali ya juu (5G-A) katika miji mbalimbali, ikiwemo Beijing na Shanghai, ikiashiria mafanikio makubwa katika kasi na muunganisho wakati ambapo waendeshaji wa huduma za mawasiliano ya simu wakiboresha ufikaji huduma katika njia za sabwei, maeneo ya kibiashara na vijijini.

5G-A pia inaitwa jina la 5.5G na baadhi ya watengenezaji na inawakilisha uboreshaji zaidi wa 5G na hatua kuelekea muunganisho wa 6G. Inatoa maboresho makubwa katika uwezo, kasi, muda wa kuunganisha, na nafasi na ni hadi mara 10 zaidi ya 5G katika suala la kasi ya intaneti.

Kwa mujibu wa wafanyakazi kutoka kampuni kuu zinazoendesha mawasiliano ya simu nchini China, modeli nyingi za simu janja za kawaida kwenye soko tayari zinalandana na mitandao ya 5G-A, ikiruhusu watumiaji kufurahia kasi ya haraka bila kutozwa gharama za ziada.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha