EAC yafanya juhudi za kuharakisha utekelezaji wa mkakati wa kikanda wa biashara ya mtandaoni

(CRI Online) Mei 13, 2025

Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) imesema imeamua kuharakisha utekelezaji wenye ufanisi wa Mkakati wa Biashara Mtandaoni wa EAC ili kuwezesha kanda hiyo kupata faida kubwa katika mabadiliko ya kidijitali.

Katika taarifa yake jana Jumatatu, EAC imesema, uamuzi huo umefikiwa kwenye mkutano uliofanyika tarehe 8 hadi 9 Mei mjini Kampala, Uganda, ambao ulithibitisha mpango wa hatua za kutunga sheria za biashara za mtandaoni na kuboresha chombo cha kufuatilia na kutathmini utekelezaji wa Mkakati wa Biashara Mtandaoni wa EAC.

Taarifa hiyo imesema mkakati huo ulioanzishwa tarehe 12 Julai, mwaka 2022, unatumika kama mpango wa kujenga mazingira ya biashara mtandaoni yenye uhai, salama na jumuishi katika Afrika Mashariki, ukilenga kuunganisha nchi wanachama katika uchumi wa kidijitali duniani.

Lengo kuu la mkakati huo ni kuanzisha soko moja la kidijitali ndani ya EAC ambapo wafanyabiashara na wateja wanaweza kuwasiliana bila vikwazo kati ya mipaka ya nchi.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha