Mwenyekiti wa Kamisheni ya AU asema utulivu na mafungamano ni muhimu kwa Afrika

(CRI Online) Mei 13, 2025

Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika (AU) Mahmoud Ali Youssouf amezungumzia vipaumbele muhimu vya uongozi mpya, akisisitiza umuhimu wa kuboresha amani na usalama, kuendeleza mafungamano ya bara hilo, na kuhamasisha rasilimali za ndani ili kufadhili maendeleo ya Afrika.

Akizungumza na waandishi wa habari kwa mara ya kwanza tangu kushika wadhifa huo, Bw. Youssoufu amesema vipaumbele katika uongozi wake wa awamu ya kwanza ya miaka minne vinaendana na mahitaji ya dharura ya kuongeza kasi ya utekelezaji wa mpango wa pili wa miaka 10 wa Ajenda ya mwaka 2063.

Akizungumzia changamoto za amani na usalama, Bw. Youssouf ameeleza hatua zinazoendelea za kufikia suluhu ya kudumu ya hali ya usalama mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), amani na usalama nchini Somalia, mvutano unaoongezeka nchini Sudan Kusini, na pia mapigano yanayoendelea nchini Sudan.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha