Jukwaa la kimataifa la kuweka vigezo kwa bidhaa za hedhi lafanyika nchini Kenya

(CRI Online) Mei 13, 2025

Mkutano wa mwaka wa kuweka vigezo vya kimataifa kwa bidhaa za hedhi umeanza jana Jumatatu katika mji mkuu wa Kenya, Nairobi, ukikutanisha watunga sera, mamlaka za usimamizi wa kanuni, wajasiriamali na wataalamu wa jinsia.

Mkutano huo ulioitishwa na Mfuko wa Udhibiti wa Afya na Usafi wa Umoja wa Mataifa (SHF), Mamlaka ya Viwango ya Kenya, na Taasisi ya Viwango ya Sweden, na Shirika la Kimataifa la Kuweka Viwango (ISO), utaendelea hadi Ijumaa wiki hii, ukiwa na lengo la kuanzisha vigezo vya kimataifa kwa bidhaa zinazotumika wakati wa hedhi.

Wakati wa mkutano huo, SHF na washirika wake wataandaa kikao cha ngazi ya juu kujadili jinsi nchi na kampuni katika nchi husika zinavyoweza kujiandaa kwa ufanisi kwa matumizi ya vigezo vinavyotambulika kimataifa vya bidhaa za hedhi.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha