

Lugha Nyingine
Rais Xi atangaza mpango wa kuzidisha ushirikiano na nchi za LAC
Rais Xi Jinping wa China akihudhuria kwenye ufunguzi wa mkutano wa nne wa mawaziri wa Jukwaa la China na CELAC (Jumuiya ya Nchi za Latin Amerika na Caribbean) na kutoa hotuba muhimu kwenye Kituo cha Mikutano cha Kitaifa cha Beijing, China Mei 13, 2025. (Xinhua/Yin Bogu)
BEIJING - Rais wa China Xi Jinping ametangaza jana Jumanne kuanzishwa kwa mipango mitano ya kusukuma mbele maendeleo na ustawi wa pamoja na nchi za Latin Amerika na Caribbean (LAC). Mipango hiyo mitano ambayo inahusisha mshikamano, maendeleo na ustaarabu na amani pamoja na mawasiliano ya kitamaduni imetangazwa na Rais Xi alipokuwa akitoa hotuba kwenye ufunguzi wa mkutano wa nne wa mawaziri wa Jukwaa la China na CELAC (Jumuiya ya Nchi za Latin Amerika na Caribbean) mjini Beijing.
Mwaka 2015, Rais Xi na wajumbe wa LAC walihudhuria ufunguzi wa mkutano wa kwanza wa mawaziri wa Jukwaa hilo la China na CELAC mjini Beijing, ambapo walitangaza uzinduzi rasmi wa jukwaa hilo.
Kuhusu Mpango wa Mshikamano, Rais Xi amesema China inapenda kuimarisha mshikamano na nchi za LAC na kuendelea kuungana mkono katika masuala yanayohusu maslahi yao ya msingi na masuala makubwa yanayofuatiliwa, kulinda kithabiti mfumo wa kimataifa ambao kiini chake ni Umoja wa Mataifa, na kulinda utaratibu wa kimataifa uliowekwa kwenye msingi wa sheria za kimataifa, na kutoa sauti kwa pamoja katika masuala ya kimataifa na kikanda.
Kuhusu Mpango wa Maendeleo, Rais Xi amesema China inapenda kujiunga na nchi za LAC katika kutekeleza Pendekezo la Maendeleo ya Dunia, kushikilia kithabiti mfumo wa biashara wa pande nyingi, kuhakikisha minyororo ya viwanda na ya utoaji bidhaa duniani iliyo tulivu, isiyozuiliwa, na kuhimiza mazingira ya kimataifa ya uwazi na ushirikiano.
Kuhusu Mpango wa Ustaarabu, Rais Xi ametoa wito wa utekelezaji wa pamoja wa Pendekezo la Ustaarabu wa Dunia, akiongeza kuwa pande zote mbili zinapaswa kushikilia mawazo kuhusu usawa, kufundishana, kufanya mazungumzo, na ujumuishi kati ya nchi zenye ustaarabu mbalimbali, kutetea maadili ya pamoja ya binadamu ya amani, maendeleo, haki, usawa, demokrasia na uhuru, na kuimarisha mawasiliano na kufundishana kiustaarabu kati ya China na LAC na kufanya mkutano wa mazungumzo ya kiustaarabu kati ya China na LAC.
Kuhusu Mpango wa Amani, Rais Xi ametoa wito wa utekelezaji wa pamoja wa Pendekezo la Usalama wa Dunia, akisema kwamba pande zote mbili zinapaswa kushirikiana kwa karibu zaidi katika udhibiti wa majanga, usalama wa mtandao, mapambano dhidi ya ugaidi, mapambano dhidi ya ufisadi, udhibiti wa dawa za kulevya na kupambana na uhalifu wa kimataifa wa kupangwa ili kulinda usalama na utulivu katika kanda.
Kuhusu Mpango wa Mawasiliano ya Kiutamaduni, Rais Xi amesema katika miaka mitatu ijayo, China itazitolea nchi wanachama wa CELAC nafasi 3,500 za ufadhili wa masomo wa serikali, fursa 10,000 za mafunzo nchini China, nafasi 500 za Ufadhili wa Masomo wa Kimataifa wa Walimu wa Lugha ya Kichina, fursa 300 za mafunzo kwa wataalamu wa kupunguza umaskini, na nafasi 1000 zilizolipiwa kupitia ufadhili wa mpango wa Daraja la Lugha ya Kichina, na kuanzisha miradi 300 ya kujipatia kipato “midogo lakini mizuri” na kuunga mkono nchi wanachama wa CELAC katika kuendeleza elimu ya lugha ya Kichina.
"China imeamua kutoa msamaha wa visa kwa nchi tano za LAC, na itapanua sera hiyo kwa nchi nyingi za kikanda kwa wakati mwafaka," Rais Xi amesema.
Gustavo Petro, Rais wa Colombia, ambaye pia ni mwenyekiti wa zamu wa CELAC, Rais wa Brazil Luiz Inacio Lula da Silva, Rais wa Chile Gabriel Boric, na Dilma Rousseff, Rais wa Benki Mpya ya Maendeleo na rais wa zamani wa Brazil, walihutubia ufunguzi wa mkutano huo mtawalia.
Rais Xi Jinping wa China akiwa katika picha ya pamoja na wageni waliohudhuria kwenye ufunguzi wa mkutano wa nne wa mawaziri wa Jukwaa la China na CELAC (Jumuiya ya Nchi za Latin Amerika na Caribbean) kwenye Kituo cha Mikutano cha Kitaifa cha Beijing, China Mei 13, 2025. (Xinhua/Ding Haitao)
Rais Xi Jinping wa China akihudhuria kwenye ufunguzi wa mkutano wa nne wa mawaziri wa Jukwaa la China na CELAC (Jumuiya ya Nchi za Latin Amerika na Caribbean) kwenye Kituo cha Mikutano cha Kitaifa cha Beijing, China Mei 13, 2025. (Xinhua/Xie Huanchi)
Rais Xi Jinping wa China na wageni wakihudhuria kwenye ufunguzi wa mkutano wa nne wa mawaziri wa Jukwaa la China na CELAC (Jumuiya ya Nchi za Latin Amerika na Caribbean) kwenye Kituo cha Mikutano cha Kitaifa cha Beijing, China Mei 13, 2025. (Xinhua/Shen Hong)
Rais wa Colombia Gustavo Petro, ambaye pia ni mwenyekiti wa zamu wa Jumuiya ya Nchi za Latin Amerika na Caribbean (CELAC) akitoa hotuba kwenye ufunguzi wa mkutano wa nne wa mawaziri wa Jukwaa la China na CELAC mjini Beijing, Mei 13, 2025. (Xinhua/Shen Hong)
Rais wa Brazil Luiz Inacio Lula da Silva akitoa hotuba kwenye ufunguzi wa mkutano wa nne wa mawaziri wa Jukwaa la China na CELAC (Jumuiya ya Nchi za Latin Amerika na Caribbean) mjini Beijing,Mei 13, 2025. (Xinhua/Yin Bogu)
Rais wa Chile Gabriel Boric akitoa hotuba kwenye ufunguzi wa mkutano wa nne wa mawaziri wa Jukwaa la China na CELAC (Jumuiya ya Nchi za Latin Amerika na Caribbean) mjini Beijing, Mei 13, 2025. (Xinhua/Yin Bogu)
Dilma Rousseff, Rais wa Benki Mpya ya Maendeleo na rais wa zamani wa Brazil akitoa hotuba kwenye ufunguzi wa mkutano wa nne wa mawaziri wa Jukwaa la China na CELAC (Jumuiya ya Nchi za Latin Amerika na Caribbean) mjini Beijing, Mei 13, 2025. (Xinhua/Yin Bogu)
Upandaji mahindi waingia kipindi cha kilele katika Mkoa wa Mongolia ya Ndani, China
UNESCO latoa wito upya wa kuimarishwa ulinzi wa maeneo ya urithi ya Afrika
Maonyesho ya Kimataifa ya Baiskeli ya China 2025 yaanza Shanghai
Shaolin Kungfu, chombo muhimu cha mawasiliano ya Utamaduni wa China na ulimwengu wa nje
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma