Peng Liyuan na mke wa Rais wa Brazil watembelea Jumba Kuu la Sanaa za Maonesho la China

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Mei 14, 2025

Peng Liyuan, Mke wa Rais wa China Xi Jinping, na Rosangela Lula da Silva, Mke wa Rais wa Brazil Luiz Inacio Lula da Silva, wakitembelea Jumba kuu la Sanaa za Maonesho la China (NCPA) mjini Beijing, Mei 13, 2025. (Xinhua/Gao Jie)

BEIJING - Peng Liyuan, Mke wa Rais wa China Xi Jinping, na Rosangela Lula da Silva, Mke wa Rais wa Brazil Luiz Inacio Lula da Silva, wametembelea Jumba Kuu la Sanaa za Maonesho la China (NCPA) mjini Beijing jana Jumanne. Rosangela ameambatana na rais wa Brazil katika ziara yake ya kiserikali nchini China.

Peng na Rosangela walizunguka kujionea usanifu wa ndani wa jumba hilo, kutazama maonyesho ya mafanikio ya "Hatua ya Utukufu," na kufahamishwa kuhusu kazi ya jumba hilo katika kuhimiza mawasiliano ya kitamaduni ya kimataifa na uenezi wa maonesho ya sanaa.

Baadaye Peng alimwalika Rosangela kutazama maonesho ya sehemu za opera maarufu, pamoja na maonesho ya kwaya za nyimbo za Kichina na Kibrazili.

Peng amesema kuwa China na Brazil ni nchi muhimu katika utamaduni, mawasiliano ya kitamaduni kati ya pande hizo mbili yamekuwa yakifanyika zaidi katika miaka ya hivi karibuni, na maelewazo na urafiki kati ya watu wa nchi hizo mbili vimekuwa vikizidishwa siku hadi siku.

Pia ameelezea matumaini kwamba pande zote mbili zitadumisha mwelekeo huo mzuri na kuwezesha watu wa nchi hizo mbili kuwa karibu zaidi.

Kwa upande wake Rosangela amemshukuru Peng kwa ukarimu wake mzuri, na kusifu wasanii kwa maonesho yao murua.

Amesifu sana mafanikio ya maendeleo ya China na utamaduni wa China unaong'aa, na kueleza nia yake ya kufanya juhudi za kuhimiza mawasiliano ya kitamaduni kati ya nchi hizo mbili, na kuendelea kuchangia katika kuzidisha urafiki kati ya Brazil na China. 

Peng Liyuan, Mke wa Rais wa China Xi Jinping, na Rosangela Lula da Silva, Mke wa Rais wa Brazil Luiz Inacio Lula da Silva, wakitembelea  Jumba kuu la Sanaa za Maonesho la China (NCPA) mjini Beijing, Mei 13, 2025. (Xinhua/Ding Lin)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha