China yarekebisha ushuru kwa bidhaa zinazoagizwa kutoka Marekani kuanzia leo Jumatano

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Mei 14, 2025

BEIJING - China imerekebisha ushuru kwa bidhaa zinazoagizwa kutoka Marekani kuanzia leo Jumatano saa 6 mchana, Kamati ya Ushuru wa Forodha ya Baraza la Serikali la China imetangaza jana Jumanne.

Kamati hiyo imeeleza kuwa, China itarekebisha ushuru wa nyongeza za bidhaa za Marekani uliotangazwa katika Tangazo la No.4 la mwaka 2025 la Kamati ya Ushuru wa Forodha ya Baraza la Serikali la China, na kusitisha utekelezaji wa asilimia 24 ya ushuru huo kwa muda wa siku 90, huku ikibakiza kiwango cha ushuru huo wa nyongeza kuwa cha asilimia 10.

Kamati hiyo imeeleza kuwa, China pia itaondoa marekebisho ya viwango vya ushuru wa nyongeza yaliyowekwa kwenye uliowekwa kwenye tangazo No. 5 na tangazo No. 6 yaliyotolewa na Kamati ya Ushuru wa Forodha ya Baraza la Serikali la China Aprili 9 na 11, mtawalia.

Katika matangazo ya mwezi uliopita yaliyotajwa hapo juu, China ilipandisha ushuru wa nyongeza kwa bidhaa zinazoagizwa kutoka Marekani hadi asilimia 84 na asilimia 125, mtawalia, ikiwa ni hatua za kulipiza kwa "ushuru wa kutozana sawa" wa Marekani.

Kamati hiyo imesema, kupunguzwa kwa ushuru huo wa forodha wa pande mbili kunalingana na matarajio ya wazalishaji na wanunuzi wa nchi hizo mbili, na kunasaidia mawasiliano kati ya China na Marekani katika sekta za uchumi na biashara, pamoja na maendeleo ya uchumi wa dunia. 

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha