

Lugha Nyingine
China yakabidhi uwanja wa michezo kwa Chad
Balozi wa China nchini Chad, Wang Xining amemkabidhi Waziri wa Vijana na Michezo wa Chad Maide Hamit Lony ufunguo wa Uwanja wa Michezo wa Mandjafa uliojengwa na China.
Akizungumza katika hafla ya kukabidhi uwanja huo juzi Jumatatu, Bw. Lony amesema uwanja huo si tu ni jengo, bali ni matunda halisi ya mfano na ushirikiano wa kivitendo kati ya Chad na China.
Amesema ushirikiano kati ya pande hizo mbili umeimarika zaidi katika miaka iliyopita katika moyo wa uhusiano wa kuheshimiana, kuaminiana na kunufaishana.
Naye Balozi Wang amesema uwanja huo ni ushuhuda wa uhusiano wa pande mbili kati ya watu wa China na Chad, na uhusiano wa kimkakati kati ya China na Chad.
Upandaji mahindi waingia kipindi cha kilele katika Mkoa wa Mongolia ya Ndani, China
UNESCO latoa wito upya wa kuimarishwa ulinzi wa maeneo ya urithi ya Afrika
Maonyesho ya Kimataifa ya Baiskeli ya China 2025 yaanza Shanghai
Shaolin Kungfu, chombo muhimu cha mawasiliano ya Utamaduni wa China na ulimwengu wa nje
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma