

Lugha Nyingine
Rwanda yawa mwenyeji wa jukwaa juu ya mageuzi katika sekta ya usafiri wa anga barani Afrika
Wajumbe wanaohudhuria Mkutano wa 13 wa Wadau wa Usafiri wa Anga na mkutano wa 2 wa Usalama na Operesheni za Usafiri wa Anga barani Afrika unaofanyika Kigali, mji mkuu wa Rwanda, wametoa wito wa mageuzi, ushirikiano wa kikanda na matumizi ya teknolojia za kiuvumbuzi ili kufungua fursa za usafiri wa anga barani Afrika na kuimarisha usalama katika bara hilo.
Mkutano huo wa siku tatu unaofanyika chini ya kaulimbiu ya “Uendelevu, Shirikiana, Vumbua na Kuimarisha Utamaduni wa Usalama barani Afrika,” umeandaliwa na serikali ya Rwanda kwa kushirikiana na Shirikisho la Mashirika ya Ndege Afrika (AFRAA).
Waziri Mkuu wa Rwanda Edouard Ngirente amesema, sekta ya usafiri wa anga ina fursa kubwa ya kuchochea mageuzi ya kiuchumi katika bara la Afrika, akiongeza kuwa usafiri wa anga unachukua nafasi muhimu katika kuendeleza ukuaji wa uchumi, kutoa nafasi za ajira, na mafungamano ya kikanda, pia inaunganisha watu, tamaduni, na masoko, na kuchukuliwa kama kichocheo cha utalii, biashara na uwekezaji.
Upandaji mahindi waingia kipindi cha kilele katika Mkoa wa Mongolia ya Ndani, China
UNESCO latoa wito upya wa kuimarishwa ulinzi wa maeneo ya urithi ya Afrika
Maonyesho ya Kimataifa ya Baiskeli ya China 2025 yaanza Shanghai
Shaolin Kungfu, chombo muhimu cha mawasiliano ya Utamaduni wa China na ulimwengu wa nje
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma