

Lugha Nyingine
Jukwaa la Wakurugenzi Afrika lafunguliwa nchini Cote d’Ivoire
Mkutano wa 12 wa Jukwaa la Wakurugenzi Afrika umeanza Jumatatu wiki hii katika mji mkuu wa Cote d’Ivoire, Abidjan, chini ya kaulimbiu ya “Je Inawezekana Makubaliano Mapya kati ya Serikali na Sekta Binafsi Kulipatia Bara Mkono wa Kushinda?”
Karibu wafanyabiashara 2,500 na maofisa wa umma kutoka nchi zaidi ya 75 wanashiriki katika mkutano huo, ambao unalenga kuanzisha makubaliano mapya kati ya nchi za Afrika na wafanyabiashara ili kuongeza kasi ya mageuzi ya kiuchumi katika bara hilo.
Akizungumza katika ufunguzi wa mkutano huo, Rais wa Cote d’Ivoire Alassane Ouattara ametoa wito kwa watunga sera barani Afrika kufikiria upya mifumo ya uratibu kati ya sekta binafsi na sekta ya umma.
Mkutano huo wa siku mbili ulilenga katika juhudi za kuboresha uongozi, kuboresha sera za umma, na kuongeza kasi ya utekelezaji wa Eneo la Biashara Huria la Afrika.
Upandaji mahindi waingia kipindi cha kilele katika Mkoa wa Mongolia ya Ndani, China
UNESCO latoa wito upya wa kuimarishwa ulinzi wa maeneo ya urithi ya Afrika
Maonyesho ya Kimataifa ya Baiskeli ya China 2025 yaanza Shanghai
Shaolin Kungfu, chombo muhimu cha mawasiliano ya Utamaduni wa China na ulimwengu wa nje
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma