Rais wa Mali asaini amri ya kufuta vyama vyote vya siasa

(CRI Online) Mei 14, 2025

Rais wa Mali Jenerali Assimi Goita amesaini amri jana Jumanne, akitangaza kufutwa kwa vyama vyote vya siasa na taasisi za kisiasa nchini humo.

Kwa mujibu wa ripoti za vyombo vya habari vya nchi hiyo, Baraza la Taifa la Mpito la Mali lilikutana Jumatatu wiki hii na kupiga kura kupitisha rasimu ya azimio la kufuta "Sheria ya Katiba ya Vyama vya Kisiasa" na "Sheria ya Hadhi ya Makundi ya Upinzani".

Serikali ya mpito ya Mali ilikutana jana Jumanne kupitia rasimu hiyo, na Rais Goita alisaini amri hiyo baada ya mjadala wa mkutano maalum wa Baraza la Mpito la Serikali.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha