

Lugha Nyingine
Finland yarudisha sanaa ya kale ya kihistoria kwa Benin
COTONOU – Waziri wa Sayansi na Utamaduni wa Finland Mari-Leena Talvitie amekabidhi rasmi Katakle – stuli ya kifalme ya sherehe kutoka Ufalme wa Kale wa Dahomey – kwa Waziri wa Utalii, Utamaduni na Sanaa wa Benin Jean-Michel Abimbola jana Jumanne.
Hafla ya kurudisha stuli hiyo imefanyika katika Ikulu ya Benin jijini Cotonou, mji mkuu wa kiuchumi wa nchi hiyo, ambapo uonyeshaji kwa umma stuli hiyo ya Katakle ulipokelewa kwa shangwe na pongezi kutoka kwa wawakilishi wa nchi zote mbili.
" (Katakle) Inaonekana ndogo, lakini inabeba uzito mkubwa wa kiishara," amesema Abimbola, akiongeza kuwa Benin sasa inatazamia juhudi nyingine za urudishaji wa sanaa za kale vilevile kuimarishwa ushirikiano wa kitamaduni, kiuchumi na kisayansi na Finland.
Kwa upande wake, Talvitie amesisitiza kuwa kurudishwa kwa Katakle kunawakilisha utambuzi wa thamani yake ya kihistoria kwa Benin. "Kazi hii inapeleka uhusiano kati ya nchi zetu mbili kwenye ngazi mpya," amesema.
Katakle ni stuli ya kifalme yenye miguu mitatu ambayo kijadi ilitumiwa kwenye sherehe za kutawazwa kwa mfalme kuashiria mamlaka, umoja, na utulivu. Stuli hiyo iliporwa kwa mara ya kwanza na wakoloni wa Kifaransa mwaka 1892 na baadaye ilikusanywa na Jumba la Makumbusho ya Kitaifa ya Finland mwaka 1939.
Novemba 2021, kwa ombi la serikali ya Benin, Ufaransa ilirudisha kazi 26 kati ya 27 za sanaa za kale zilizoporwa wakati wa ukoloni.
Upandaji mahindi waingia kipindi cha kilele katika Mkoa wa Mongolia ya Ndani, China
UNESCO latoa wito upya wa kuimarishwa ulinzi wa maeneo ya urithi ya Afrika
Maonyesho ya Kimataifa ya Baiskeli ya China 2025 yaanza Shanghai
Shaolin Kungfu, chombo muhimu cha mawasiliano ya Utamaduni wa China na ulimwengu wa nje
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma