Rais wa China afanya mazungumzo na rais wa Chile

(CRI Online) Mei 15, 2025

Asubuhi ya tarehe 14, Mei, rais Xi Jinping wa China kwenye Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing akikutana na rais Gabriel Boric wa Chile, ambaye yupo nchini China kuhudhuria mkutano wa nne wa mawaziri wa Jukwaa la China na CELAC. (Li Xiang/Xinhua)

Rais Xi Jinping wa China Jumatano amekutana na rais wa Chile Gabriel Boric ambaye yupo nchini China kuhudhuria Mkutano wa Nne wa Mawaziri wa Jukwaa la China na CELAC (Jumuiya ya Nchi za Latin Amerika na Caribbean).

Katika mazungumzo na Rais Boric, rais Xi ameeleza kuwa, China iko tayari kuimarisha imani ya kisiasa na Chile, kushikilia kuheshimiana, kutendeana kwa usawa na kunufaishana, na kuimarisha kubadilishana uzoefu wa utawala.

Kwa upande wake, rais Boric ameeleza matumaini ya kuimarisha ushirikiano na China katika sekta za biashara, uwekezaji, teknolojia ya AI, na kujenga kwa pamoja “Ukanda Mmoja, Njia Moja” kwa ubora wa juu.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha