Rais wa China afanya mazungumzo na rais wa Colombia

(CRI Online) Mei 15, 2025

Asubuhi ya tarehe 14, Mei, rais Xi Jinping wa China kwenye Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing akikutana na rais Gustavo Petro wa Colombia, ambaye yupo nchini China kuhudhuria mkutano wa nne wa mawaziri wa Jukwaa la China na CELAC. (Huang Jingwen/Xinhua)

Rais Xi Jinping wa China Jumatano amekutana na rais wa Colombia Gustavo Petro ambaye yupo nchini China kuhudhuria Mkutano wa Nne wa Mawaziri wa Jukwaa la China na CELAC (Jumuiya ya Nchi za Latin Amerika na Caribbean).

Wakati alipokutana na rais Petro, rais Xi amesisitiza kuwa inapaswa kutumia fursa ya Colombia kujiunga rasmi na familia ya ujenzi wa “Ukanda Mmoja, Njia Moja”, kuimarisha ushirikiano kati ya nchi hizo mbili kwenye kiwango cha juu zaidi.

Naye rais Petro amesisitiza kuwa pande hizo zinapaswa kuimarisha imani ya kisiasa na kusaidiana, kujenga kwa pamoja “Ukanda Mmoja, Njia Moja”, na kuimarisha ushirikiano katika sekta za biashara, miundo mbinu, nishati mpya na AI, ili kuboresha maisha ya wananchi.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha