Wizara ya Mambo ya Nje yasema hatua za China dhidi ya “Ushuru wa fentanyl” wa Marekani zitaendelea kufanya kazi

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Mei 15, 2025

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Lin Jian tarehe 14 alipojibu swali kwenye mkutano na waandishi wa habari alisema, upande wa Marekani uliongeza kwa raundi mbili ushuru wa forodha kwa bidhaa za China kwa kutumia kisingizio cha fentanyl, na China imechukua hatua za kupinga mara moja, zikiwemo hatua za ushuru na zisizo za ushuru, ili kulinda kithabiti haki yake halali. Hatua hizi sasa zinaendelea kufanya kazi.

Mwandishi wa habari kwenye mkutano huo aliuliza kuwa, habari zimesema baada ya mazungumzo ya ngazi ya juu kuhusu uchumi na biashara kati ya China na Marekani yaliyofanyika Geneva, upande wa China utapunguza ushuru kwa bidhaa za Marekani kutoka asilimia 125 hadi 10 ndani ya siku 90, huku upande wa Marekani ukipunguza ushuru kwa bidhaa za China hadi asilimia 30, ambayo asilimia 20 ni ushuru wa nyongeza kwa sababu ya fentanyl. Je, China ina maoni gani kuhusu hali hiyo?

Lin Jian alisema, China na Marekani zilifikia makubaliano mbalimbali mazuri katika mazungumzo huko Geneva, zikikubaliana kupunguza kwa kiasi kikubwa ushuru kwa pande zote mbili. Upande wa Marekani umeahidi kuondoa asilimia 91 ya ushuru, na kusitisha utozaji wa asilimia 24 ya “ushuru wa kutozana kwa usawa (ushuru wa reciprocal)”; Na China pia inaondoa asilimia 91 ya ushuru wa kupinga na kusitisha utekelezaji wa aisilimia 24 ya ushuru huo. Pande zote zimebakiza ushuru wa forodha wa asilimia 10.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha